Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Washindi
wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo
wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika
jijini Mwanza.
Washindi
wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo
wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika
jijini Mwanza.
Meneja
Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Cocacola mkoani Mwanza Samwel
Makenge,(kushoto) akimkabidhi pikipiki Marysiana Kijita, baada ya
kushinda promosheni ya ‘ Mchongo chini ya kizibo’ wakati wa hafla ya
makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Wakazi wa kanda ya ziwa na mikoa jirani mambo yanazidi kuwanyokea
kutokana na kuendelea kujishindia zawadi za pikipiki,Televisheni bapa za
kisasa ,fedha taslimu na zawadi nyinginezo kupitia promosheni ya
Coca-Cola inayoendelea ijulikanayo kama ‘Mchongo chini ya kizibo’
Wiki iliyopita washindi wa pikipiki 6 walikabidhiwa zawadi zao sambamba
na washindi 2 wa televisheni wakiwemo wengine wengi waliojishindia fedha
taslimu na t-shirt kutoka kampuni ya Coca-Cola.
Waliokabidhiwa
pikipiki ni Derick Magnus (Nyakato), Ismail Hamis (Magu), Joseph Mafuru
(Mahina Mwanza) Pendo (Bariadi Mkoani Simiyu), Daniel Keheta
(Mkolani),na Marysiana Kijita (Hungumalwa).Waliokabidhiwa televisheni ni
Rhoda Joel, Marco Kitula.
Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao
waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye lengo la
kuinua maisha ya wateja wake “Nimefurahi kujishindia pikipiki kutoka
Coca-Cola nitaitumia katika shughuli za biashara ili kuongeza kipato cha
familia yangu”
Alisema
Marysiana Kijita,kwa furaha.
Derick Magnus alisema kuwa amefurahi kujishindia zawadi ya pikipiki
kupitia promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’na kudai kuwa
itamrahisishia usafiri wake binafsi na familia yake “Chombo hiki
kitarahisisha usafari katika shughuli zangu za ujasiriamali sambamba na
usafiri kwa familia yangu”.Alisema.
Mmoja wa washindi wa televisheni,Marco Kitula ,alisema kuwa zawadi
aliyojishindia imekuja kwa wakati mwafaka ambapo ataweza kuona matukio
mengi na michezo mbalimbali kupitia televisheni yake ya kisasa
aliyojishindia “Napenda sana kuangalia matukio kupitia luninga na
michezo mbalimbali nitaburudika vizuri na familia na marafiki”.Alisema
kwa furaha.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika
kiwanda cha Nyanza mwishoni mwa wiki ,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni
hiyo, Japhet Kisusi,amesema kuwa promosheni hii ambayo imeandaliwa kwa
ajili ya kuboresha maisha ya wateja wanaotumia bidhaa za kampuni
inaendelea vizuri na washindi wanaendelea kukabidhiwa zawadi zao.
Aliwataka wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuendelea kuchangamkia
promosheni kupitia kunywa soda za kampuni ya Coca-Cola na kuongeza kuwa
zawadi bado ziko nyingi.”Mchongo Chini ya Kizibo inawezesha kujishindia
zawadi nono za fedha taslimu,bodaboda,televisheni aina ya SONY LED,kofia
na soda za bure.
Alisisitiza
kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho
laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu
kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa
zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu
vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa
Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia,
T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini
ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.
0 comments:
Post a Comment