Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilayani ya Ukerewe likiendelea, pichani ni baadhi ya wananchi wa kata ya Kakelege wakisubiri zoezi la kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia.
Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndg. Zabron Rusohoka akiwaelekeza baadhi ya wananchi taratibu wanazopaswa kuzifuata wakati wa ujazaji fomu za maombi ya Wilayani Ukerewe.
Umati wa wananchi wa Kata ya Ukerewe kijiji cha Nakatunguru wakisubiri huduma ya Usajili wakati zoezi la Usajili likiendelea Wilayani humo.
Usajili
Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mwanza na wilaya zake umepamba
moto, ambapo wananchi kutoka Wilaya za Kwimba, Ukerewe, Ilemela,
Misungwi na Sengerema wamejitokeza kwa wingi kusajili. Kwa wananchi wa
Wilaya Nyamagana, taratibu za kuanza kwa Usajili zinaendelea ambapo
wataanza usajili rasmi wiki hii.
Katika
kufanikisha zoezi hilo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
Halmashauri na Manispaa pamoja na Watendaji wa mitaa/Vijiji
wamejizatiti kwa dhati kuhakikisha zoezi hili linafanyika na kukamilika
kwa wakati uliopangwa. Aidha; Wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi
kusajiliwa kutokana na manufaa mapana ya zoezi hilo kwa mwananchi mmoja
mmoja na kwa Taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment