Mhe Masala ametoa pongezi hizo akiwa katika ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu wilayani Ilemela.
"Lengo ni kufuatilia namna fedha zimetumika kwani tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia" amesema Mhe Masala
Pamoja na pongezi hizo, Mhe Masala amemtaka Mkurugenzi kupitia fedha za mapato ya ndani, kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ambayo yalijengwa kwa nguvu za wananchi.
Nae Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Angeline Mabula amemshukuru Mhe Rais kwa namna ambavyo amekuwa akigusa sekta mbalimbali ndani ya jimbo lake hususan sekta ya elimu kwani imepunguza mzigo mkubwa kwa wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
"Kupitia Rais Samia kazi imerahisishwa hakuna tena uchangishaji wa fedha za ujenzi wa madarasa kero hii imeondoka", Amesema Mhe Mabula
Bi Ummy Wayayu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela nae ameungana na viongozi wengine kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo huku akiwasihi wataalam wanazisimamia fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.
"Niendelee kuwasihi kuwa fedha ya serikali zinapoletwa tuzisimamie, kwa kuzingatia thamani ya fedha inaonekana hii iende pamoja na kutunza nyaraka mbalimbali za manunuzi",amesistiza Bi Ummy
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mhe Renatus Mulunga kwa niaba ya wananchi wa Ilemela ameishukuru serikali chino yake Mhe Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha za utelezaji wa niradi huku akihimiza juu ya suala ya ushirikiano.
Shilingi Bilioni 2.46 zilipokelewa kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya, ukamilishaji wa maboma sambamba na ujenzinwa matundu ya vyoo katika shule 25 za sekondari wilayani Ilemela.
Home »
» DC MASALA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU
DC MASALA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Masala ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Ilemela kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi wa vyumba 44 vya madarasa katika shule za sekondari.
0 comments:
Post a Comment