Home » » MAONI YA KILA MTU NI MUHIMU KATIKA MCHAKATO MAANDALIZI YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

MAONI YA KILA MTU NI MUHIMU KATIKA MCHAKATO MAANDALIZI YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

Katibu tawala wa Wilaya ya Ilemela Adv.Mariam Msengi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Hassan Masala amesema hakuna mtu wala kundi litakaloachwa katika mchakato wa maandalizi ya dira ya taifa ya 2050,ni mpango wa serikali ya awamu ya sita kuhakikisha wananchi wote wanashiriki mchakato huo.

Amezungumza hayo wakati wa kongamano la maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 ambapo maoni yamekusanywa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wawakilishi wa wazee,watu wenye ulemavu,vijani ,asasi zisizo za kiserikali ,vyama vya siasa,vyama vya kijamii,viongozi wa dini ya wakristu na waislamu,wanamichezo na wamachinga.

Akiwasilisha taarifa fupi ya mafanikio ya dira ya maendeleo 2025 mratibu wa ukusanyaji maoni ya dira ya taifa Ilemela Joseph Mrimi ameainisha malengo makuu ya dira ya taifa ikiwemo kuboresha hali ya maisha ya Watanzania,kuwepo kwa mazingira ya amani,utulivu na umoja,kujenga utawala bora na utawala wa sheria sambamba na kujenga uchumi imara unaoweza kuhimili ushindani kutoka mataifa mengine.

Aidha Adv.Msengi amesema ushiriki wa wananchi na makundi yote ya wadau una manufaa makubwa kwa taifa kwani inajenga uaminifu na kukuza hisia za umiliki kwao sambamba na kuakisi maono ya pamoja .

“ Maendeleo yaliyopatikana yanatokana na nchi kutekeleza  mipango na mikakati ya muda mrefu ,muda wa kati na muda mfupi katika nyanja za kiuchumi na kijamii tangu dira 2025ilipozinduliwa.”

Shekh Abdulwarith Juma Abdallah ni shekhe wa Wilaya ya Ilemela maoni yake juu ya dira ya taifa ni matamanio kwamba ifikapo mwaka 2050 Tanzania iwe na huduma zilizoboreshwa huku akisisitiza uwajibikaji hasa kwa watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kuhudumia watu kutoa huduma kwa weledi na uadilifu na kupinga rushwa .

Nae Mwenyekiti wa Democratic Party (DP ) wilaya ya Ilemela Mchungaji Clement Masonyi amesema Dira ya maendeleo ijayo iangalie maboresho ya mitaala ya elimu ili kuondoa dhana ya wasomi wengi kutegemea kuajiriwa na badala yake watoto wajengewe uwezo wa kujitegemea tangu shule za msingi.

Akihitimisha kongamano hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Wayayu amesema ana imani kubwa na maoni mengi yaliyotolewa na wadau hao huku akiahidi baadhi ya maoni ambayo yapo ndani ya uwezo wa manispaa kuanza kutekelezwa mara moja katika kuboresha .


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa