Zikiwa
zimebaki siku chache kabla ya siku inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki
wa soka Jijini Mwanza,Pamba Day,kampeni yake imezidi kuwabamba mashabiki
baada ya kufunguliwa tawi jipya huko Buchosa wilayani Sengerema.
Tawi
hilo la mashabiki wa Pamba Jiji FC limefunguliwa leo Agosti Mosi,2024
na katibu Tarafa wa kata ya Kahunda,Joseph Kapunda kwa niaba ya mkuu wa
wilaya hiyo na kusisitiza huo ni muendelezo wa kufunguliwa matawi zaidi
wilayani humo.
"Tuna wajibu wa kushikamana kwa vitendo kuiunga
mkono timu yetu ya Pamba Jiji FC ambayo mbali na burudani imekuja kuinua
uchumi wa mkoa wetu,"Kapunda.
Amesema siku ya Pamba Day
itadhihirisha furaha ya mashabiki kwa timu yao kwa kuujaza kwa wingi
uwaja wa CCM Kirumba na mechi zote za ligi kuu ya NBC.
"Tulimsikia
Mkuu wetu wa Mkoa Mhe Said Mtanda akituhimiza kushikamana na tuwe
wachezaji wa 12 uwanjani siku zote za michuano ya timu ya Pamba Jiji
akimaanisha kuishabikia uwanjani",amesisitiza katibu Tarafa wakati
akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa Pamba
Jiji FC.
Mwenyekiti mteule wa tawi hilo Salawe
Magembe amebainisha atahakikisha kwa kushirikiana
na wanachama wenzake wanazidi kuliimarisha tawi hilo na kuwa wakereketwa
wa kweli kwa timu ya Pamba Jiji FC
Mchezaji wa zamani wa Pamba
miaka ya 90 ambaye alikuwa mlinda mlango Madata Lubigisa amewataka
mashabiki wa soka kuhakikisha timu yao inadumu katika ligi hiyo na kuwa
tishio kwa timu za uzito wa juu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Nimefurahi
mlivyo hamasika na timu yenu ya Wana Kawekamo TP Lindanda,Pamba Jiji FC
ufunguzi wa tawi hili uwe msingi bora wa kupanga mikakati mbalimbali ya
kuipa maendeleo timu yenu,"Agnes Magubu,kiongozi wa Kampeni ya Pamba
Day
Kampeni hiyo inayoendelea kwenye wilaya zote za Mkoa wa
Mwanza inakwenda Pamoja na uuzwaji wa tiketi za kuingilia siku ya Pamba
Day na jezi za timu hiyo.
Home »
» KAMPENI YA PAMBA DAY YAZIDI KUPAMBA MOTO,TAWI LA WANACHAMA LAFUNGULIWA BUCHOSA
0 comments:
Post a Comment