Tone

Tone

TEMESA YAKABIDHIWA BOTI NNE ZA KISASA BAADA YA UJENZI WAKE KUKAMILIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ukodishaji na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle, nyuma yao ni Meneja wa TEMESA mkoani Mwanza Mhandisi Ferdnand Mishamo wakati wa majaribio ya boti Mpya ya MV Mkongo  iliyojengwa kwa ajili ya kutumika katika eneo la Utete Rufiji Mkoani Pwani. Boti hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 40.
 Boti tatu kati ya nne mpya zilizokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Makabidhiano yamefanyikia jijini Mwanza na boti hizo zitasafirishwa kuelekea Pangani Tanga, Kilambo Mtwara na Msangamkuu Mtwara ili zianze kutoa huduma kwa wananchi.
  Boti Mpya ya MV Kuchele iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria nane na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Msangamkuu Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
 Boti Mpya ya MV Tangazo  iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria 25 na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Kilambo Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
 
Na Theresia Mwami – TEMESA Mwanza
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, leo amepokea boti nne zilizokuwa zikijengwa na kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza. Dkt. Mgwatu amesema kukamilika kwa boti hizi ni utekelezaji wa ahadi za Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa alizozitoa kwa wananchi wa Pangani Tanga pamoja na Kilambo na Msangamkuu Mtwara kwa nyakati tofauti.
Dkt. Mgwatu ameongeza kuwa boti hizo nne zitatoa huduma za dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala wakati vivuko vikubwa vinapokuwa haviwezi kutoa huduma kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupungua kwa kina cha maji katika maeneo ya Kilambo mkoani Mtwara pamoja na Utete Mkoani Pwani.
Nae Mkurugenzi kutoka kampuni ya Songoro Marine Boatyard Mhandisi Major Songoro amesema kuwa boti tatu kati ya nne zilizokabidhidhiwa zimejengwa kwa kutumia “fibre Glass” na boti moja imejengwa kwa kutumia chuma. Boti ya MV Kuchele ambayo itapelekwa katika eneo la Msangamkuu Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria nane, sawa na boti ya MV Bweni itakayopelekwa katika eneo la Pangani mkoani Tanga. MV Mkongo itakayopelekwa Utete mkoani Pwani ina uwezo wa kubeba abiria 40 na MV. Tangazo itakayopelekwa Kilambo/Namoto Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria 25.
Aidha Dkt. Mgwatu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuwezesha ujenzi wa boti hizo na tayari amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha anazisafirisha boti hizo kwenye maeneo husika haraka iwezekanavyo ili wanachi waanze kunufaika na huduma mbadala itakayotolewa na boti hizo. Ujenzi wa boti hizo umefanywa kwa kutumia fedha za ndani na umegharimu jumla ya shilingi milioni 415.
Mwisho

MWANAHABARI GEORGE BINAGI WA LAKE FM MWANZA AUAGA UKAPELA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jana jumapili March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.

Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.

"Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. 

Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani, hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.

BMG inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za kanisani.

MWANAHABARI GEORGE BINAGI NA MISS PENDO KISAKA KUUAGA UKAPELA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa mtandao wa Binagi Media Group, George Binagi (kulia) pamoja na Miss Pendo Kisaka (kushoto), wanatarajiwa kufunga pingu za maisha masaa machache yajao.

Wapendanao hao wanafunga ndoa hii leo March 26,2017 majira ya saa nane mchana katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, na baadae kufuatiwa na hafla itakayofanyika Ukumbi wa Sun City Hotel uliopo Ghana Green View Jijini Mwanza kuanzia majira ya saa moja jioni.

Zifuatazo ni picha za hafla ya kumuaga bibi harusi mtarajiwa (Sendoff) iliyofanyika ijumaa iliyopita March 17,2017 Jijini Dar es salaam.
Sifa na Utukufu ni kwa Mwenyezi Mungu, Amina!

MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika Jijini Mwanza.

Judith Ferdinand, BMG
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.

Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo  pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.

Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.

Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442  lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza  kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.

Kwa upande wake  Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye  mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.

Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina  wataalamu wake.

"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.

Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo  cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.

Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
Displaying Pix.JPG

USIKU WA MISS PENDO KISAKA NA MWANAHABARI GEORGE BINAGI WAFANA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jana ijumaa March 17,2017 kuamkia leo jumamosi, ilikuwa ni siku muhimu kwa Malikia wa nguvu, Pendo Kisaka, ambapo ndugu, jamaa na marafiki zake walijumuika naye kwenye Sendoff yake kuelekea kwenye ndoa anayotarajiwa kufunga na mwanahabari/ mwanablogu, George Binagi, March 26,2017 Jijini Mwanza.

Shughuli ilifanyika katika ukumbi wa Heinken, Mbagala Kijichi Jijini Dar es salaam. Ni mwendeleo wa kuelekea kwenye ndoa takatifu ya wawili hao iliyotangazwa March 12,2017 kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
BMG
Bibi harusi mtarajiwa akimvisha saa mmewe mtarajiwa
Bibi harusi mtarajiwa (kulia) na best lady wake (kushoto)
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake na kusema ahsante kwa malezi yenu bora
Bibi harusi mtarajiwa, Pendo Kisaka (katikati), akimtambulisha mmewe mtarajiwa, George Binagi (kushoto)

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa