Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu akipanda mti katika eneo la Soko la Kimataifa la Samaki Kirumba jijini Mwanza, akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za NSSF katika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kupitia Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri. Kampeni ya utoaji elimu inaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Mipango Haistaafu na Mazingira Hayana Likizo.”
Home »
» WAZIRI SANGU ASHIRIKI UPANDAJI MITI KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI KIRUMBA MWANZA

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)




0 comments:
Post a Comment