Home » » KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA BUNDA, IMETEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA BUNDA, IMETEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Mtelela siku ya tarehe 26/7/2024 ameongoza kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea na kukagua kituo cha Afya Hunyari, nyumba za watumishi 3 in 1 zilizopo katika kituo cha Afya Hunyari, mradi wa maji Sanzate, mradi wa barabara kutoka Kiloleri Nyabuzume yenye urefu wa km 4.1, kiwanda cha vijana Moto, kilichopo Kijiji cha Mariwanda, pamoja na shule ya Sekondari Mariwanda.

Ndugu Mtelela alimuagiza meneja RUWASA wa Wilaya kuhakikisha anaongeza kasi katika ukamilishaji wa Ujenzi wa sehemu za wananchi kuchotea maji (DPs), ili waweze kupata huduma ya maji haraka na kwa ukaribu, wakati walipotembelea mradi wa maji Bukama, na Sanzante.

Pia, alimuagiza Mhandisi wa TARURA  Wilaya kuhakikisha anakamilisha barabara hiyo kwa kuhakikisha anatengeneza vizuri sehemu ambayo magari yatakuwa na uwezo wa kugeuza.

Kamati ilimpongeza meneja wa TANESCO Wilaya kwa kuweza kufikisha umeme katika shule ya Sekondari Mariwanda, na kumuagiza kuhakikisha anapeleka umeme katika kiwanda cha vijana Moto, ili waweze kuendelea na shughuli za kiuchumi katika kiwanda hicho kwani saivi wanashindwa kuendelea sababu ya kukosa umeme wa kuendeshea mitambo ya mashine.

Katika ziara hiyo waliongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, wakuu wa Taasisi husika, RUWASA, TARURA, na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa