Tone

Tone
Home » » UJENZI WA KIVUKO KIPYA KIGONGO BUSISI WAANZA RASMI

UJENZI WA KIVUKO KIPYA KIGONGO BUSISI WAANZA RASMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akiwa ameshikilia vifaa vya kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akichomelea vyuma kuashiria kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.




Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Meneja wa miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Bwana Salehe Songoro (wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) mojawapo ya malighafi itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)

Na Alfred Mgweno (TEMESA MWANZA)

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, ameshiriki katika zoezi la kuweka msingi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. 

Zoezi hilo linaloashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo limefanyika Pasiansi katika eneo linalotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli, vivuko na boti linalomilikiwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Mwanza iliyoshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.9 za kitanzania. 

Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mhandisi Amos Mutahiwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bwana Salehe Songoro Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro, na wafanyakazi wa Kampuni ya Songoro na wale wa TEMESA.

Akiongea baada ya zoezi hilo, Dkt. Mgwatu amesema wakazi wa Mwanza wana kila sababu ya kujivunia kuanza kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani kitakapokamilika kitasaidia kurahisisha usafiri wa abiria na mali zao na hivyo kuimarisha uchumi wao. Aidha Dk. Mgwatu amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kujenga kivuko ndani ya muda uliopangwa kwenye mkataba na kuzingatia ubora wa hali ya juu. 

Pia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za maendeleo kwa ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro ameahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati huku akisisitiza kuwa kampuni yake imejipanga vyema kufanya kazi kwa kasi kwa kuwa malighafi kwa ajili ya ujenzi wa kivuko tayari ipo kwenye eneo la ujenzi.

Kivuko hicho kipya kitakapokamilika kitafanya idadi ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la Kigongo Busisi kufikia vinne vikiwemo vile vya MV. Sengerema, MV. Misungwi, pamoja na MV. Sabasaba.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa