Tone

Tone
Home » » RPC MSANGI AWAASA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI ILI KULINDA AMANI YA NCHI

RPC MSANGI AWAASA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI ILI KULINDA AMANI YA NCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na David John Mwanza

JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limewaasa waandishi wa habari nchini,  kuhakikisha wanatumia kalamu zao kwa uweledi na uadilifu mkubwa katika kuhabarisha umma, mambo muhimu ya nchi na kwamba waepuke kutumiwa na watu wachache ambao mara zote hawalitakii mema Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Rpc Ahmed Msangi (pichani) wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ambaye aliongozana na Naibu katibu mkuu wa Taasisi ya kutetea haki za binadamu nchini TAHURA Habibu Rajabu jana.
Kamanda Msangi mbali na mambo mengine alisema kuwa waandishi wa habari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa salama kwani kama kalamu zao zitatumika vibaya ni rahisi kuvunja usalama ambao umejengwa na waasisi wa Taifa.
"Nitowe wito kwa waandishi wa habari ni vema wakaongeza uzalendo na uchungu kwa nchi yao na hasa kuhakikisha mnatumia kalamu zenu kwa ustadi wa hali ya juu na kuepuka kutumiwa na watu ambao hawalitakii mema taifa,".alisema Msangi.
Aliongeza kuwa katika suala la kulinda amani linatakiwa kwa kila mtanzania, kwani hata mwandishi wa habari ni mtanzania na pindi usalama utakapokosekana haitajalisha nafasi ya mtu hivyo lazima waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wazalendo la kuhakikisha wanapigania taifa lao kwa nguvu zote.
Msangi alifafanua kuwa watanzania wasidanganywe kwani uhuru ambao unapatikana hapa nchini huwezi kupata mahala pengine popote hivyo ni lazima kujiepusha na watu ambao wanataka kujipatia umaalufu kwa mgono wa watu wengine wakiwemo wandishi wa habari.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa