Home » » NAIBU WAZIRI WA ARDHI AZUNGUMZA NA WAKAZI WA ILEMELA

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AZUNGUMZA NA WAKAZI WA ILEMELA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Judith Ferdinand, Mwanza

Wananchi  mkoani Mwanza wametakiwa kulipa kodi ya ardhi na majengo kwa wakati ili kuepuka usumbufu, kwani serikali ya awamu ya tano imejikita  kusimamia sheria, kanuni na taratibu kwa maendeleo ya taifa.

Agizo hilo limetolewa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula wakati akihitimisha ziara yake ya kusikiliza kero, kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo la Ilemela katika mkutano uliofanyika Mtaa wa Nenetwa, Kata ya Nyamanoro.

Mabula alisema kila mwananchi anawajibu wa kulipa kodi kwa wakati kwani ulipaji wa mwaka huu umefanyika vizur ingwa kulikuwa na baadhi ya adha kadhaa ikiwemo wananchi kushinda kwenye mistari tangu asubuhi hadi jioni na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Alisema ulipaji kodi hufanyika kuanzia  Julai Mosi hadi Juni 3o ya kila mwaka hivyo wananchi wana muda wa kutosha kulipa kulipia kodi zao hivyo siyo vyema kusubiri siku za mwisho.

“Sisi wana Mwanza tunatakiwa  kuwa mstari wa mbele kulipa kodi kwa wakati, kwa sababu husaidia serikali kufanya mambo ya  maendeleo, pia tusimuangushe mlezi wetu Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu aliejitolea kuwa mlezi wa wilaya yetu ya Ilemela”. Alisema Mabula na kuongeza;

“Zile kamati za mipango za halmashauri zinapaswa kuangalia waliolipa kodi na ambao bado ili kuwakumbusha na kuondoa adha ya msongamano na hili liende sambamba na kodi zingine kwani tunapata shida sisi wenyewe wakati sheria zipo, nisingependa kuona mwana Ilemela shitakiwa kwa sababu ya kodi ya ardhi ama majengo”. Alisisitiza Mabula.

Aidha Mabula aliwaomba wananchi kulipia gharama za upimiwaji wa viwanja kwa ajili ya zoezi la urasimilishaji makazi ili waweze kupata hati
 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa