Afisa mkuu wa masoko na mauzo wa TTCL Bw. Peter Ngota akiongea na wateja wa TTCL katika hafla hiyo.
wafanyakazi wa TTCL katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo.
Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na ujumbe alioongozana nao.
mgeni rasmi akiongea na mameneja wa TTCL kutoka mikoa mbalimbali kwa kutumia "Bongo phone" katika huduma ijulikanayo kama "Conference call" ambayo iliwavutia wateja wengi waliohudhuria hafla hiyo. anayefuata baada ya mkuu wa mkoa (kulia) ni Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mhe. Halifa Hassan Hida.
******
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa kwa kwa kutoa huduma na bidhaa za uhakika hususani huduma ya intanet.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Evarist Ndikilo wakati
wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na TTCL kwa ajili ya
wateja wake wa mkoa wa Mwanza.
Amesema
TTCL ndio mhimili mkuu wa mawasiliano hapa nchini na ni ukweli ulio
wazi kuwa Watanzania wengi wanaiona TTCL kuwa tegemeo lao la kwanza
katika Mawasiliano hapa nchini
Aidha
amesema “pamoja na huduma bora za mawasiliano mnazotoa, bado mna
changamoto ya kuboresha zaidi mtandao wenu kwani kuna baadhi ya maeneo
ambayo hayana mtandao wa TTCL hivyo kuwanyima fursa wananchi wazalendo
kutumia huduma hii ambayo pia ni ya kizalendo ili kuimarisha uchumi wa
nchi yetu. Tunatambua juhudi mnazofanya katika kuwafikia wateja zaidi
maeneo ua vijijini, tafadhalini ongezeni kasi katika jambo hili.”
Akijibu
baadhi ya maoni kutoka wateja, Afisa mkuu wa masoko na mauzo wa Kampuni
ya Simu Tanzania TTCL Bw. Peter Ngota amesema pamoja na mafanikio mengi
tuliyoyapata TTCL, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni
pamoja na Wizi au hujuma katika njia zetu za mawasiliano yaani nyaya na
mikonga ya simu katika maeneo mbali mbali mkoani hapa na kusababisha
wateja wetu kukosa mawasiliano na kupata usumbufu usio wa lazima.
Mbaya
zaidi kuna baadhi ya maeneo hapa Mwanza wamefikia hatua kutumia nyaya
za TTCL kujiunganishia umeme kwa njia zisizo halali, jambo ambalo ni
hatari kwa uhai wao na watu wanaowazunguka pia wanaisababishia kampuni
na taifa hasara kubwa kupitia hujuma hii.
Kukatika
mara kwa mara kwa Mkongo wa taifa kunakosababishwa na shuguli za
kibinadamu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara n.k. ; tunawaomba
wananchi wa Mwanza kuachana na vitendo vya hujuma na kuwa waangalifu
wakati wa shughuli zao za kijamii na maendeleo ili kuepuka uharibifu
kwenye njia za mawasiliano.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema, akiwa kama
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa mwanza,
atahakikisha miundombinu ya TTCL inalindwa kwa kuwaagiza vyombo vya
usalama kuhakikisha mtandao huu hauhujumiwi ili kuleta maendeleo kwa
wateja na wa TTCL na wananchi kwa ujumla.
Kwa hisani ya Michuzi Media
Kwa hisani ya Michuzi Media
0 comments:
Post a Comment