Mwanza
ASIKALI
polisi wakike wametakiwa kujituma na kuonyesha ushujaa wa
hali ya juu wakati wakitimiza majukumu yao ili kuienzi
kwa vitendo kauli mbiu ya wanawake tunaweza.
Mkuu
wa wilaya ya Ukerewe, Mwanza Mery Tesha amewambia washiliki wa afla
fupi iliyoandaliwa na jumuia ya asikali polisi wa
wilaya hiyo ya kumuaga mmoja wa asikali hao
aliyestaafu kuwa wakati umefika sasa kauli hiyo
ienziwe kwa vitendo.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika
ukumbi wa mikutano wa Millenia Praza mjini Nansio mbali
ya kumpongeza asikali huyo wa kike aliyetumikia
jeshi hilo kwa miaka 39 alitaka asikali wengine wa
kike kujenga tabia ya ushuja.
Alisema
mbali ya nidhamu pia asikali wa majeshi yote
wa ikiwemo polisi wa jinsia zote wanatakiwa kuonyesha
ujasili na weledi katika utendaji wao ili kuthibisha uwezo wa
mwanamke katika kutenda kazi.
Akifafanua
Tesha aliwataka asikali polisi wakike waliopokazini
kuelewa kuwa asikali huyo aliyestaafu akiwa tayari ametunukiwa
nishani tatu alijituma na hata pengine alijitoa wakati
wa kulinda usalama wa wananchi na kutaka waige mfano wake ili pia
hapo baada wafikie mafanikio kama hayo.
Mstaafu
huyo Talkisia Kitambi mbali ya kupata nishani
tatu ikiwemo ya ushiliki wa vita ya kagera ya mwaka
1979 iliyomwondoa Rais wa Uganda Idd Amin Dada
madaraka pia anayo taaluma ya Uuguzi.
Katika
risala yake iliyowasilishwa na Inspekta wa polisi
Emanuel Onyango alisema Talkisia aliyestaafu kwa mjibu wa
sheria za utumishi wa umma tayari amefanikiwa kupanda
hadi cheo cha mkaguzi msaidizi wa polisi.
Imebainishwa
kuwa mbali ya nishani ya kushiliki vita ya Kagera
pia ametunukiwa na Amiri jeshi mkuu nishani
nyingine mbili za utumishi wa muda mrefu pamoja na nishani
ya ushujaa wa kulenga shabaha akitumia sira za moto.
Alifafanua
kuwa nishani ya kulenga shabaha aliipa mwaka 1987
baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano
yaliyofanyika jijini Nairobi na kushilikisha asikali polisi
wa nchi tatu za Afrika mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania.
Wakizungumza
kabla ya kufungwa kwa afla hiyo mmewe ambae ni mkuu wa polisi
[OCD] wa wilaya hiyo Shitambi Shilogile na
mkewe Talkisia wameshukulu na kutaka jamii
kuendelea kushilikiana polisi kukabili vitendo vya
uhalifu.
0 comments:
Post a Comment