Helikopta maalum iliyowabeba
viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe pamoja
na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili eneo la Mnada
Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wilayani
humo mwishoni mwa Juma.
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman
Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza mwishoni
mwa juma kwenye mkutano wa hadhara.
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele
umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao
wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama
kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh.
John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema wilayani
Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Na. Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Chama cha
Domekrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh.FREEMAN MBOWE amewataka Watanzania
kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya ili ipatikane Katiba
itakayokidhi haja ya Watanzania.
Amesema hayo alipokuwa
akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani waMwanza alipokuwa
kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa chama hicho kuunga
mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwepo Serikali tatu
siyo mzigo kama Chama cha Mapinduzi (ccm) kinavyosema ila tunataka
kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na ile ya muungano ili kuleta
usawa ndani ya Muungano huo.
Pia amesema kuwa Lugha ya
Kiingereza na Kiswahili ipatiwe kipaumbele kufundishwa kuanzia daraja la
awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea Watanzania kufahamu Lugha ya
Kiingereza vema na kupata ajira kwa urahisi.
(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
0 comments:
Post a Comment