Mwandishi wetu, Ukerewe-Mwanza Yetu
MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza Dr. Leonard Masale ametakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo la umasikini linalowakabili wakazi wa wilaya hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya hiyo Bi, Mery Tesha
Akionekana kushutushwa na hali ya umasikini inayowakabili wakazi wa wilaya hiyo alisema hatakubali kuona tatizo hilo linaendelea wakati viongozi wa wilaya hiyo na mkoa wakibaki bila kubuni na kuanzisha miradi ya kulitatua matatizo yanayowakabili wa kazi wa wilaya hiyo.
Alisema wakati wilaya nyingine za mkoa wa Mwanza wakazi wake wanakipato cha wasitani ya sh. 926,000 kwa mwaka katika wilaya ya Ukerewe pato la mwananchi ni wasitani wa sh. 340,000.
Alisema wasitani wa kipato cha mkazi wa Ukerewe unaonyesha kuwa kwa siku anapata sh. 800 kiasi ambacho ni chini ya makisio ya pato la taifa la sh. 1,500 kwa mtanzania kwa siku .
Kufuatia hali hiyo amemuagiza Dk. Masale kubuni miradi yenye tija ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo Ufugaji nyuki, kilimo na kuhakikisha pato la uvuvi linapatika na kuwanufaisha wakazi wa wilaya hiyo.
Akieleza zaidi Pinda alisema wakati asilimia 90 ya wilaya hiyo ni eneo la maji ya ziwa Victoria lakini pato linalotokana na rasilimali hiyo aliwanufaishi wakazi wake na kutaka juudi za makusudi zichukuliwe ili wananchi waondokane na umasikini uliokkisili.
Naye Dr. Masale alisema hatua mbali mabali za kukabiliana na tatizo hilo zinafanyika ikiwemo kuboresha ufugaji pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji bora pamoja na kutoa mbegu bora za mazao ya chakula na biashara zinazoimili magonjwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment