Na John Maduhu, Mwanza
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amemmwagia sifa Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, kuwa ni mmojawapo wa vijana wachapa kazi na jasiri na kumfananisha na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, aliyewahi kujiuzulu uwaziri.
Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Sengerema katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sengerema, wakati akiwa katika ziara ya kuitembelea wilaya hiyo.
Aliwataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanamtumia Ngeleja kuwaletea maendeleo na kueleza kuwa Taifa bado linamuhitaji kutokana na mchango wake.
Alisema katika jambo la nadra kutokea hapa nchini, baada ya Ngeleja kuondoka katika Baraza la Mawaziri kutokana na mabadiliko yaliyofanywa alimuandikia barua Rais Jakaya Kikwete na kumshukuru kutokana na kumuamini na kumsaidia kama Waziri wa Nishati na Madini kwa muda wa miaka mitano.
“Kwa kufanya hilo, Ngeleja alionyesha ujasiri wa hali ya juu, hivyo namfananisha na mzee wetu, Rais Mwinyi ambaye aliamua kujiuzulu nyadhifa alizokuwa nazo, ingawaje hakuhusika na jambo lolote lililokuwa limetokea na baadaye alikuja kuwa rais.
“Chama na Serikali baada ya kuona kelele zimezidi viliamua kuchukua hatua kwa wale waliokuwa wakilalamikiwa ingawaje hawakuhusika na lolote, lengo lilikuwa ni kuondoa malumbano, mimi nimekuwa mshauri mkuu wa Ngeleja pia namuamini ni mchapa kazi mzuri,” alisema Pinda.
Alisema katika kuhakikisha Serikali inaondoa kero za wananchi wa Sengerema, tayari Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 350 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi aliyekuwa akijenga kilomita tano za barabara za Sengerema na kueleza itaongeza kilomita nyingine nne za lami.
Alisema Serikali inatarajia kuweka lami nyepesi kwa barabara ya Kamanga- Sengerema yenye urefu wa kilomita 35 kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Sengerema.
Kuhusu maji, alisema Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanatarajia kuupatia Mji wa Sengerema majisafi na salama katika mradi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo utawanufaisha wakazi wa Nyatukala, Mwabaruhi, Tabaruka na Nyampulukano.
Awali, Ngeleja alimueleza Pinda kuwa wananchi wa Sengerema wanakabiliwa na tatizo sugu la majisafi na salama na kuiomba Serikali kuhakikisha inatatua tatizo hilo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment