Na Derick Milton Mwanza.
Watumishi wa serikali mkoani mwanza wameiomba serikali kuwatengea mda muhafaka ili kuweza kutoa maoni yao kama watu wengine kwa kukutana na tume na sio kutuma mesegi kwa nija ya simu au email kama walivyoambiwa.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala msaidizi utawala na utumishi mkoani mwanza Bi.Crescencia Joseph wakati akifanya maojiano na gazeti hili kuhusu maandalizi kwa watumishi wa serikali katika kutoa maoni kuhusu katiba mpya.
Amesema kuwa watumishi wa serikali wote walikuwa wameiomba serikali kuwapa mda muhafaka wa kuweza kwenda katika mikutano mbalimbali amabayo itakuwa imeandaliwa na tume ili kweza kutoa maoni yao.
“Kuna tatizo lilijitokeza kwa watumishi wetu ukiangalia mda wa tume ambao itautumia kukaa katika mkoa wetu na kukusanya maoni umekuwa ni mda ambao hauwapi watumishi wetu fursa ya kwenda kwenye mikutano na kuanza kuchangia, mda wote watatakiwa kuwa makazini kwao na mda tume inaohutumia ni mfupi sana hauwezi kusabanbisha mtu kuacha kazi nyingi na kuanza kwenda kutoa maoni”
“Tuliweza kukaa na watumishi na kuwaeleza hivyo na bahati nzuri waliweza kuelewa na tuliweza kuwapa utaratibu wa watumishi jisi gani watashiliki bila ya kutoenda makazini kwao kwa kutumia simu pamoja na mitandao nyingine kama email ambapo mawasiliano yote hayo tuliweza kuwapatia na kuwaeleza jinsi gani watatuma.”
Tume ya katiba imeanza kazi yake rasmi ya kukusanya maoni katika mkoa wa mwanza kuanzia tarehe 27/8/2012 hadi tarehe 31/9/2012 ambapo imeanzia katika wilaya ya Sengera na itamalizia katika wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza siku hiyo ya tarehe 31/08/2012.
Akizungumzia maadalizi kwa ajili tume hiyo pamoja na jinsi gani wananchi watashiliki katika mchakato huo Bi Cresencia amesema kuwa maandalizi yote yameisha kuwa tiyari kwa maana ya vituo vya mikutano kwa kushilikiana na wakuu wa wilaya pamoja na wenyeviti wa halmashauli na wakurugenzi kwa maana ya kuhamasisha wananchi wao ili kuweza kushiliki ipasavyo katika zoezi hilo.
“Ofisi ya mkuu wa mkoa imewaagiza wakuu wa wilaya ,wenyeviti wa halmashauli pamoja na wakurugenzi kuweka maandalizi mazuri ya kutolea maoni na hata kuwahamasisha wananchi kwa njia mbalimbali ili kuweza kushiliki ipasavyo”.
Amewataka wananchi kutumia fursa hii waliyopewa na serikali kwa kutoa kero zao walizonazo na kuaacha kulalamika tu katika vyombo vya habari na hata mikutanoni kwani itakuwa haina haja ya kuweza kufikisha kero zao panapostaili.
0 comments:
Post a Comment