Home » » SITA MBALONI KWA KUGOMA KUHESABIWA MWANZA

SITA MBALONI KWA KUGOMA KUHESABIWA MWANZA

                                       Na Derick Milton Mwanza.
Jeshi la polisi  mkoani mwanza linawashikilia watu sita kwa  kosa la kugoma kehesabiwa katika zoezi zima la sensa ambalo linaendelea kwa nchi nzima sasa.
Akitoa taarifa hiyo  mbele ya waandishi wa habari kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani mwanza kamanda Liberatus Barlow amesama kuwa jeshi hilo limekamata watu hao katika sehemu tofauti tofauti katika mkoa wa mwanza kwa kushawishi na hata kugoma kuhesabiwa.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Omary Shedraka[30] msukuma makazi wa kirumba wilaya ya Ilemela jijini mwanza,Mohamed Idd[28] mwalimu makazi wa kiloleli jijini mwanza  pamoja na Samora Khasuman[26] wote hawa wakiwa wamekatwa katika wilaya ya ukelewe mkoani mwanza.
Wengine aliowataja kamanda Barlow ni Mohamed Fakuru[48] mkazi wa kisesa wilayani magu mkoani mwanza  kwa kosa la kuwazuia makarani wahesabu familia yake,Bashiru Athumani [29] muha mkazi wa ibanda kirumba jijini mwanza naye kwa kosa la kukataa kuhesabiwa na makarani wa sensa pamoja naye Cpriany Mohamed[41] mkazi wa kapri point jijini mwanza.
Aidha kamanda Barlow ameongeza kuwa jeshi la polisi linamtafuta mtu mmoja aliye julikana kwa jina moja tu la Kasimu mkazi wa kirumba jijini mwanza kwa kosa la kukataa kuhesabiwa na kisha kukimbia  na kutokomea pasipo kujulikana.
Kamanda Barlow  amewataka wananchi mkoa wa mwanza kutoa ushilikiano kwa makarani pamoja na wenyeviti wamtaa ili kufanikisha zoezi zima la sensa linalotegemea kumalizika siku ya juampili.
Amesema kuwa watuhumiwa wote wamefikishwa mahakani ili  kuweza kujibu kesi zinazowakabili.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa