Na huu ndio muonekano wa kiwanda hicho kwa nje.
Na
hapa ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi! Baada ya kukagua
kinu cha kukobolea mpunga Waziri Mhagama na wadau wengine walipata
wasaa wa kutembelea eneo lingine la kiwanda hicho ambapo kwa mujibu wa
Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige
ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi chenye uwezo kusaga
mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku.
Ukafika
wasaa wa kufafanua mradi huo. Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa bodi ya
nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (aliesimama)mkopo huu
utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku
na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa
uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi.
Vinu hivyo vinavyofufuliwa kwa mkopo wa NSSF vilisimamisha uzalishaji
wake tangu mapema miaka ya 1990 baada ya kushindwa kujiendesha.
Ikawa
ni pongezi tu kwa NSSF na Serikali kwa kufanya kile kilichoshindikana
kwa miongo ya miaka!Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw Stanislaus Mabula
akitoa shukrani zake kwa naiba ya wananchi wa jimbo hilo pamoja na
wakazi wa Mwanza kwa ujumla. Pamoja na faida nyingine nyingi, kufufuliwa
kwa kiwanda hicho kunatajwa kuwa kutazalisha ajira zaidi ya 340 za
moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa
moja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (wa pili
kushoto) Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) ikiwa ni mkopo kutoka Shirika hilo kwenda bodi ya nafaka na
mazao mchanganyiko kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa
nafaka kilichopo jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Dk Charles Tizeba (kushoto) huku wadau wengine wakishuhudia.
Muonekano wa sehemu ya mitambo ya kiwanda hicho cha kukobolea mchele kilichopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
Hatimaye
hundi hiyo ikafika kwa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko Bw. John Maige (wa tatu kushoto). Wanaoshuhudia ni pamoja
na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (wa pili
kushoto), Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw. Stanislaus Mabula (katikati)
na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia).
Kabla
ya makabidhiano hayo Waziri Mhagama alipata wasaa kukugua mitambo ya
kinu cha kukoboa mchele kinachotarajiwa kufufuliwa kupitia mkopo huo
ambapo Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John
Maige (mbele) alimuhakikishia Waziri Mhagama na wadau wengine kuwa
kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutawezesha jumla ya tani 96 za mchele
kukobolewa kwa siku kupitia kinu hicho.
Mwanza,
Agosti 20, 2017: Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa
mkopo wa Tshs bilioni 8.99 kwenda kwa Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko ya Tanzania kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji
wa nafaka katika jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za
mfuko huo kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda hapa nchini.
Mkopo huo unalenga kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuweza kuvifufua vinu vyake viwili vya usindikaji wa mazao ya mpunga na mahindi vilivyopo mkoani humo kwa kununua vifaa na mitambo mipya na hatimaye kuanza uzalishaji baada ya kusimamisha uzalishaji huo mapema miaka ya 1990.
Mkopo huo unalenga kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuweza kuvifufua vinu vyake viwili vya usindikaji wa mazao ya mpunga na mahindi vilivyopo mkoani humo kwa kununua vifaa na mitambo mipya na hatimaye kuanza uzalishaji baada ya kusimamisha uzalishaji huo mapema miaka ya 1990.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi ya mkopo huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alitoa wito kwa Wizara yenye dhamana ya kulimo hapa nchini kuisimamia vyema bodi hiyo kiutendaji ili iweze kuijendesha kwa ufanisi utakaoiwezesha kurejesha mkopo huo unaotarajiwa kulipwa ndani ya kipindi cha miaka sita (6) ikijumlisha kipindi cha mpito yaani (grace period) ya mwaka mmoja.
"Mbali na Wizara yenye dhamana ya kilimo, pia niwaombe sana uongozi wa mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa mkoa kutambua kuwa ufanisi wa kiwanda hiki unategemea sana uwepo wa malighafi ya kutosha hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha uwiano kati ya uzalishaji wa malighafi na uzalishaji wa kiwanda vinakwenda sambamba,'' alisisitiza.
Alilipongeza Shirika la NSSF kwa uwekezaji wa viwanda vyenye tija kiuchumi ndani ya muda mfupi ambapo kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hadi sasa shirika hilo limewekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiwanda cha kutengeneza viuadudu vya kuua vimelea vya mbu kiitwacho Tanzania Biolarvicide Limited kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.
"Uwekezaji wa NSSF pia unaonekana kwenye bodi ya nafaka na Mazao mchanganyiko ya Tanzania, Mkoani Dodoma, viwanda vipya vya kuzalisha sukari Mkulazi, mkoani Morogoro, kiwanda cha chaki Maswa (Maswa Chalk & General Enterprises) ambacho kipo Simiyu...hongereni sana!'' alipongeza.
Waziri Mhagama alitumia wasaa huo pia kuwataka waajiri wasiolipa michango ya wanachama kuwasilisha michango hiyo kwa wakati na kwa usahihi kwani kutofanya hivyo ni kosa kisheria na kuanwanyima haki wanachama hao huku akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wale wasiotekeleza sharia hiyo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alimuhakikishia Waziri Mhagama kuwa mbali na kuisimamia kwa ukaribu bodi hiyo ili iweze kurejesha mkopo huo, wizara yake imejipanga kuhakikisha kwamba miradi yote ya kilimo inayohusisha uwekezaji kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini inasimamiwa kwa umakini, ufanisi na weledi mkubwa ili kulinda pesa ya wanachama wa mifuko hiyo.
"Kwa kutambua kwamba ufanisi wa viwanda hivi unategemea zaidi kilimo kuna mipango na mikakati mizuri kuhakikisha mnyororo wa thamani unaohusika kuzalisha malighafi za viwanda hivi haukatiki,'' alisema Waziri Tizeba.
Alitaja baadhi ya mipango na mikakati hiyo kuwa ni pamoja na ujio wa Mpango maalumu wa kuandaa mbegu bora unaotekelezwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill Gates. Alikili kuwa kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba wa mbegu bora unaotakona na utegemezi wa mbegu hizo kutoka nje ya nchi huku taifa likizalisha asilimia 35 tu ya mbegu hizo.
Waziri Tizeba alitumia fursa hiyo kutangaza uamuzi wa serikali kutoa bei elekezi kwenye pembejeo za mbolea ili kudhibiti uuzwaji kwa bei holela wa bidhaa hiyo muhimu ambapo kila mfanyabiashara alikuwa akiuza bidhaa hiyo kwa bei inayotokana na utashi wake.
"Mbolea zinahusika ni zile za kukuzia na kupandia yaani UREA na DAP ambapo kuanzia leo bei elekezi itakuwa inatangazwa kulingana na maeneo husika. Tunataraji kuwa uwepo wa bei elekezi utasaidia kupunguza bei ya mbolea hususani ya UREA kwa asilimia zaidi ya 15 kwa mfuko,'' alisema.
Alitolea
mfano kuwa katika baadhi ya mikoa bei ya mbolea ilifika hadi Sh.
100,000 lakini chini ya mfumo wa bei elekezi haitazidi sh. 56,000 kwa
mfuko huku maeneo mengine ikiwa chini zaidi ya bei hiyo.
Mapema, akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara alisema kuwa mbali na lengo la kutunza thamani ya michango ya wanachama, uwekezaji unaofanywa na shirika hilo pia unalenga kuchochea ukuaji wa shughuli mbali mbali za uchumi na kijamii ambazo pia huongeza ajira, kipato na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania walio wengi na mwishowe kuongeza wanachama wa mfuko.
"Mkopo huu utapelekea kufufua kiwanda ambacho kitaleta ajira Zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na pia kuongezeka kwa wanachama wa Mfuko,'' alibainisha.
Mapema, akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara alisema kuwa mbali na lengo la kutunza thamani ya michango ya wanachama, uwekezaji unaofanywa na shirika hilo pia unalenga kuchochea ukuaji wa shughuli mbali mbali za uchumi na kijamii ambazo pia huongeza ajira, kipato na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania walio wengi na mwishowe kuongeza wanachama wa mfuko.
"Mkopo huu utapelekea kufufua kiwanda ambacho kitaleta ajira Zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na pia kuongezeka kwa wanachama wa Mfuko,'' alibainisha.
Prof.Kahayrara alisisitiza kuwa Uwekezaji huo unafanywa kwa kuzingatia Sera ya Uwekezaji ya Shirika na Mwongozo wa Uwekezaji kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii unaotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kushirikiana na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Akitoa taarifa za kiwanda hicho,Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ndugu John Maige alisema mkopo huu utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi.
"Mkopo huu pia utawezesha kuwepo kwa soko la uhakika kwa wakulima wa mahindi na mpunga hapa nchi na nitumie fursa hii kuipongeza serikali kwa hatua ya kuzuia usafirishaji wa mazao ghafi nje ya nchi.'' alipongeza Maige huku akiongeza shukrani zake kwa Mfuko wa NSSF kwa uamuzi wa kuwekeza kwenye kufufua kiwanda hicho.
0 comments:
Post a Comment