Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi
nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya
kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso.
Mbunge
wa Chilonwa Joel Mwaka akimkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo kuzungumza na wananchi katika mradi wa maji
Itiso.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wananchi na viongozi wa Itiso.
………………….
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi
wa halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi kumtafuta mkandarasi wa mradi
wa maji Itiso ili akamilishe mradi huo haraka kabla ya kuchukuliwa
hatua.
Akizungumza
leo katika ziara yake ya kukagua mradi huo, Jafo amesema mkandarasi
huyo kutoka kampuni ya Audancia anatakiwa kurudi eneo la mradi haraka
kukamilisha kama mkataba wake unavyoelekeza.
“Mmtake
arudi haraka hapa kwenye eneo la mradi au kama ikishindikana achukuliwe
hatua za kisheria kwa kukamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani
kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba,”amesema Jafo.
Amesema
Mkandarasi huyo ametoweka eneo la mradi huku akiwa amefunga mabomba
yenye ubora wa chini kwenye njia kuu (Main line) kinyume cha mkataba.
Ameeleza kuwa mkandarasi huyo amelaza mabomba ya Class B(PN 6) badala ya bomba za Class C(PN10) jambo ambalo
limesababisha mradi huo kushindwa kufanyakazi kwa kuwa mabomba yaliyofungwa yameshindwa kuhimili msukumo wa maji.
Kadhalika,
Jafo pia ameagiza mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Company
LTD kutafutwa kwani ameshindwa kusimamia mradi huo ipasavyo na
kuruhusu kazi hiyo ifanyike kinyume cha mkataba na kuruhusu mkandarasi
atoke eneo la mradi wakati vituo vinne havitoi maji kati ya vituo kumi
vya mradi.
Hata
hivyo Jafo ametoa onyo kwa wakandarasi washauri na wakandarasi wa
ujenzi wa maji ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao kwamba hivi sasa
kazi zilizo chini ya Ofisi ya Tamisemi watazisikia kwenye bomba.
“Tutakuwa
tumebaini makampuni yote yanayofanya kazi kwa ubabaishaji na
kutoyapatia kazi tena za usimamizi na ujenzi katika halmashauri
zote,”amesema Naibu Waziri Jafo
Jafo ameagiza kasoro zote za mradi huo zirekebishwe na ifikapo Septemba 15, mwaka huu mradi huo uwe umekamilika.
0 comments:
Post a Comment