Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwandishi Wetu*
Akiongea wakati wa kipindi
cha jicho letu la habari kinachorushwa na star tv Mwandishi Mwandamizi
Bw.Pascal Mayala amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakiupinga
muswada huu bila kuangalia faida zilizopo ndani yake ikiwamo uboreshwaji
wa maslahi na mafunzo kwa waandishi wa habari.
"Waandishi wa habari
wamekuwa wakikaa na kuukosoa muswada huu bila kuangalia nini kipo ndani,
kiukweli muswada huu unatotauti Sana na Sheria ya Magazeti ya mwaka
1976 tunaoutumia sasa, unafaida nyingi kwa waandishi na utawasaidia
kukua kiuandishi". Alisema Bw. Mayala.
Bw.Mayala aliongeza kuwa
muswada huu utawezesha kuwapata waandishi walioelimika kutokana na uwepo
wa vifungu vinavyowawezesha waandishi kupata mafunzo katika maeneo
yatakayowawezesha kukua kitaaluma.
Naye Mwandishi Mwandamizi
Bw.Derek Murusuri amesema kuwa Sekta ya habari nchini imekuwa na
changamoto zakiutendaji kwa muda mrefu jambo ambalo linakuja kutatuliwa
na muswada wa huduma za habari ya mwaka 2016.
Bw.Derek alisema kuwa
muswada huu kwa kiasi kikubwa umejikita kutatua chamgamoto zilizokuwa
zikiwakabili waandishi ikiwemo masuala ya mikataba na bima kwa waandishi
wa habari.
"Tumeshudia tasnia yenye
changamoto nyingi kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha muda mrefu na
malalamiko yamekuwa ni mengi hasa kwenye masuala yanayohusu maslahi ya
waandishi wa habari"-Alisema Bw.Derek.
Mwandishi wa habari Juma
mudimi amewataka waandishi wa habari kuusoma muswada huo na kuacha
kupotosha watu juu ya vifungu vilivyopo ndani ya muswada huo.
Akizungumzia kuhusu
Kuongezwa kwa muda Edwin Soko amesema suala hilo lisiwe ajenda bali
kuusoma na kuuelewa kwa maslahi ya tasnia.
Home »
» MUSWADA WA HUDUMA WA HABARI WA MWAKA 2016 UTALETA HESHIMA KWENYE TASNIA YA HABARI TOFAUTI NA ILIVYOKUWA AWALI.
0 comments:
Post a Comment