Home » » JIJI LA MWANZA LATAKIWA KUWAONDOA WATOTO OMBAOMBA MITAANI

JIJI LA MWANZA LATAKIWA KUWAONDOA WATOTO OMBAOMBA MITAANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Watoto kutoka taasisi ya "Pamoja Youth and Children Foundatio" ya jijini Mwanza wakionyesha michezo ya sarakasi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na BMG

Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kushirikiana na idara ya Ustawi wa Jamii, metakiwa kuwaondoa watoto waliozagaa mitaani ambao wamekuwa wakiomba misaada kwa wasamaria wema barabarani.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza yamefanyika shule ya msingi Mabatini, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, amesema wengi wa watoto hao wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufiwa na wazazi ama wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kimasomo, hivyo Halamshauri hiyo ina wajibu wa kuwasaidia.

Amesema hatua ya kuwaondoa watoto hao inaweza kuonekana ni ngumu kutekelezeka, lakini inawezekana ikiwa kila mdau ikiwemo jamii itatoa ushirikiano ambapo amewasihi madiwani katika baraza la halmashauri ya Jijini la Mwanza kupeleka hoja kwenye baraza lao ili jambo hilo liwekwe kwenye vipaumbele vya Halmashauri hiyo.

"Mkurugenzi, Meya na Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza, chukueni hatua kuwaondoa watoto waliozagaa mitaani ikiwemo mtaa wa Nkuruma kwani hawako pale kwa kupenda. Mkifanya hivyo itakuwa sifa kwenu na kwa baraza la madiwani la mwaka 205/20". Amesema Konisaga.

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka June,16 ikiwa ni kumbukumbu ya mauaji ya mamia ya watoto waliouawa na polisi wa kikaburu mwaka 1976 katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini wakati walipokua wakiandamana kupinga kubaguliwa kielimu kwa kufundishwa katika lugha wasiyoifahamu ya Afrikana.

Katika risala yao, watoto wameiomba serikali pamoja na jamii kuwalinda na vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ukatili unaowakumba ikiwemo kukosa elimu.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga (wa kwanza kushoto), ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, akizungumza katika maadhimisho hayo.
Halleluyah Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza, akisima risala ya watoto katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika hii leo.
Halleluyah Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza (kushoto) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Paulina Robert.
Wanafunzi wakisoma ngojera katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
Mshereheshaji kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza
Wahudhuriaji akiwemo mtoto kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza, wakiendelea kufuatilia maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga (wa tatu kushoto), wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
Kauli mbiu mkoani Mwanza

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa