Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza
SERIKALI imemtaka mkandarasi wa ujenzi wa
nyasi bandia katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kuhakikisha
ukarabati huo unakamilika haraka ili uweze kutumika.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM), aliyetaka kujua ni lini serikali itawasisitiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha uwanja huo unakamilika na kuendeleza malengo yaliyokusudiwa.
“Jimbo la Nyamagana ni jimbo pekee linalochangia mradi wa ujenzi wa nyasi bandia kupitia TFF, Sh. milioni 160,” alisisitiza mbunge huyo
Akijibu swali hilo, Wambura alisema nyasi hizo tayari zimewasili Dar es Salaam tangu Aprili 17, 2016 na baadhi ya vifaa tayari vimeshafika katika uwanja huo na mkandarasi ameshaanza kazi.
Alisema TFF sasa wako katika mchakato wa kumalizia kusafirisha vifaa vilivyobaki na kwamba ukarabati huo unahitaji umakini mkubwa ili uwe mzuri, imara na wenye hadhi ya kimataifa.
Wambura alisema mradi wa uboreshaji wa uwanja huo ulianza mwaka 2014 na kutakiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu, ukiwa na thamani ya Sh. bilioni 1.1 na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilitoa msaada kwa TFF wa Sh. bilioni 1 huku Halmashauri ya Nyamagana ilichangia Sh. milioni 192 na kwamba nyasi hizo zimegharimu tozo ya zaidi ya Sh. milioni 220.2.

Chanzo Gazeti la Nipashe
0 comments:
Post a Comment