NA JUDITH NYANGE, MWANZA
SHAURI la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe kuiomba Mahakama kubatilisha amri polisi kuuzia
mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa limepangwa kuanzwa kusikilizwa
leo.
Tofauti na yalivyokuwa maombi yaliyowasilishwa Juni 10, mwaka huu
katika shauri la namba 79 la mwaka 2016, mbele ya Mahakama Kuu Kanda
ya Mwanza yaliyowajumuisha washtakiwa watano, shauri la sasa
litajumuisha washtakiwa wawili ambao ni Kamanda wa Polisi Wilaya ya
Geita (OCD) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Shauri la awali namba 79 la mwaka 2016 liliwajumuisha washtakiwa
watano wakiwamo Kamanda wa Polisi Wilaya ya Geita na Kahama, Kamishina
wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Juni 14, mwaka huu, Jaji Mohamed Gwae, alibaini upungufu wa
sheria katika shauri hilo kwa kumjumuisha Kamishna wa Operesheni na
Mafunzo wa Polisi, Nsato Mssanzya ambaye kisheria anastahili kufunguliwa
mashtaka masijala kuu.
Jaji Gwae aliwasahauri mawakili wa Chadema kurekebisha hati yao.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza jana, Mbowe alisema shauri hilo litaanza kusikilizwa kesho
(leo) mbele ya Jaji Gwae.
Katika shauri hilo, Mbowe kupitia kwa Mawakili wake, Paul Kipeja na
John Malya amewasilisha maombi manne yanayohusu kutafuta haki ya
kufanya mikutano na mikusanyiko ya siasa iliyozuiliwa na polisi Juni 7,
kupitia kwa Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao
Makuu, Nsato Mssanzya.
Mbowe ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kutamka kuwa amri
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Geita (OCD) kuzuia mikutano
ya hadhara iliyopaswa kufanyika Katoro na mjini Geita kuwa si sahihi
na ni kinyume cha sheria.
“Ombi jingine tumeiomba mahakama kutengua amri ya OCD wa Geita
aliyoitoa Juni 7, 2016 kuzuia mikutano ya hadhara ya Chadema
iliyokuwa imetangazwa na kupangwa kufanyika wilayani humo kuanzia tarehe
hiyo, kwa muda usiojulikana.
Chanzo Gazei la Mtanzania
0 comments:
Post a Comment