Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kushoto) jana akichukua fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan akimkabidhi fomu hiyo ambayo gharama yake ni shilingi elfu hamsini.
Na:George GB Pazzo
Makada mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM
Mkoani Mwanza, wameendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchukua fomu za
kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi za
Udiwani na Ubunge.
Zaidi ya Makada sita wa chama hicho tayari
wamejitokeza na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika
jimbo la Ilemela, ambapo miongoni mwao
ni aliekuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM yaani UVCCM Wilaya ya
Misungwi John Buyamba ambae jana alichukua fomu ya kugombea.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu
hiyo, Buyamba ambae pia aliwahi kuwa ni Mjumbe wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, alisema
kuwa akipata nafasi anayoiwania atahakikisha anashirikiana na wananchi kwa
lengo la kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo
mbiundomimbu, Afya pamoja na Elimu.
Katika ngazi ya Udiwani, pia mchakato
wa Uchukuaji fomu umeendelea katika Wilaya ya Ilemela ambapo Mwenyekiti wa
UVCCM Kata ya Nyamanoro Abdulrahman Khalfan Kange nae alijitokeza na
kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika Kata hiyo na hivyo kufanya idadi ya
waliochukua fomu kufikia makada watatu.
Baada ya kuchukua fomu, Kange ambae
pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mwanza, alibainisha
kuwa akipata fursa ya kuwa diwani wa Kata ya Nyamanoro atajikita zaidi katika
kuondoa kero mbalimbali zinazoikabili Kata hiyo ikiwemo kuboresha upatikanaji
wa miundombinu ya maji pamoja na elimu.
Kwa pamoja Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi pamoja na Bahati Masoud Ramadhan ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro, waliwasihi watia nia wote waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea, kuzingatia katiba ya chama, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kuachana na siasa za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe, kwani atakaebainika kukiuka taraibu hizo, jina lake halitaweza kupitishwa na vikao vya chama.
Fomu za kuwania udiwani na ubunge
katika Chama cha Mapinduzi CCM zilianza kuchukuliwa Julai 15 na mwisho wa
kurejesha fomu hizo unatarajiwa kuwa Julayi 19, mwaka huu majira ya saa kumi za
alasiri hivyo watia nia wote wametakiwa kuzingatia muda uliopangwa.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kushoto) akilipa pesa kwa ajili ya gharama ya kuchukua fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan akipokea pesa hizo ambazo ni shilingi elfu hamsini. Aliekaa kushoto ni Khadija Iddy mkewe Kange.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Katika) akionyesha fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan na kushoto ni Khadija Iddy mkewe Kange.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) baada ya kuchukua fomu akiwa na mkewe Khadija Iddy (Kushoto).
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akiwa na mkewe Khadija Iddy (Kushoto) wakati wa kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Mbele ya Wanasa matukio, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Wa tatu kushoto) akiwa pamoja na makada na viongozi wa CCM Kata ya Nyamanoro.
Binagi Media Group Productions
0 comments:
Post a Comment