Tone

Tone
Home » » DAKTARI: MGONJWA HAKUFA KWA EBOLA

DAKTARI: MGONJWA HAKUFA KWA EBOLA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Yusuph Bwire amesema matokeo ya uchunguzi wa sampuli yaliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yanaonyesha kwamba Salome Richard hakufariki dunia kwa ugonjwa wa ebola bali kwa tatizo la ini.
Dk Bwire alisema ini lilishambuliwa na virusi na kusababisha vidonda vilivyovujisha damu sehemu mbalimbali za mwili, hali ambayo inashabihiana na dalili za ebola.
Wakati daktari akitoa taarifa hiyo, jana familia ya marehemu ililalamikia kitendo cha Serikali kukataza kufukua mwili huo ili kuuzika upya nyumbani kwao.
Malalamiko hayo yalitolewa na mume wa marehemu, Shadrack Ibrahimu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Chema Bupandwamhela, wilayani Sengerema.
Alisema yeye na ndugu zake wawili waliruhusiwa kutoka kwenye karantini Ijumaa saa 3.30 asubuhi, baada ya uongozi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema kutoa majibu ya ugonjwa huo.
“Alikuja muuguzi na mganga mkuu kutuambia ‘pole sana...majibu yamekuja yanaonyesha siyo ebola, mgonjwa alikuwa na tatizo la ini ambalo lilikuwa limeharibika’. Ndiyo tukaambiwa kuanzia siku hiyo tuko huru tukatoka wote,” alisema Ibrahimu.
Ibrahimu alisema baada ya kuruhusiwa aliomba mwili wa marehemu ufukuliwe, lakini alinyimwa na kuambiwa kwamba gharama za kuufukua hazipungui Sh520,000.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chema Bupandwamhela, Antoni Kanyala alisema Salome alionekana kuwa na homa, ndipo alipopelekwa Kituo cha Afya Mwangika.
, lakini hakupata taarifa za kuhamishiwa Sengerema hadi aliposikia habari za kifo chake.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa