Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HALMASHAURI ya wilaya ya Ukerewe
Mwanza inaendelea kubolesha mazingirana na miundombinu ya huduma
za afya ili kuvutia wataalamu lengo
likiwa kuboresha huduma hiyo kwa jamii.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya hiyo
Dr. Nyanda Kombe amesema hayo jana wakati anazungumzia miradi minne inayondelea kutekelezwa
kwa gharama ya sh. Mil. 451.
Alisema miradi inatekelezwa kwa fedha
za ruzuku ya serikali kuu kupitia mpango wa
maendeleo ya afya ya msingi [MMAM] na fedha
nyingine ikitokana na mpango wa maendeleo [CGD].
Alibainisha kuwa katika mwaka wa
fedha wa uliopita tayari wamepokea sehemu
ya fedha ya utekelezaji wa miradi hiyo ambapo hivi sasa ipo
katika hatua mbali mbali ya utekelezaji wake.
Miradi hiyo ni pamoja na jengo la Kliniki ya
uzazi na mtoto inayojengwa kwa gharama ya sh. Mil. 230 na nyumba
ya watumishi yenye makazi ya familia
mbili inayojengwa kwa gharama ya sh.
Mil. 60.
Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba ya
kufikiwa watumishi yenye uwezo wa kupokea watu sita inayojengwa kwa
gharama ya sh. Mil. 141 pamoja na jengo la kupumzikia wagonjwa wakati
wanasubili huduma linalojengwa kwa gharama ya sh. Mil.20.
Akielezea juudi zaidi za halmashauri ya
wilaya hiyo za kuboresha huduma ya afya Dr.
Kombe alisema katika mwaka ujao wa fedha pia
wameomba sh. Mil. 361.32 kwaajiri ya ujenzi wa zahanati tatu
na kituo kimoja cha afya.
Alisema kati ya fedha hizo sh.
Mil. 161 zimeombwa kwaajiri ya kujenga zahanati katika
visiwa vidogo vya Kulazu , Chibasi huku nyingine ikitakiwa
kujengwa katika kijiji cha Masonga, wakati huo sh. Mil.
200 zimembwa kujenga kituo cha afya cha mji wa Nansio.
Alisema miradi hiyo ni muimu na kuongeza kuwa mbali
ya kuvutia watumishi pia inaweka mazingira mazuri ya
utoaji huduma za tiba hasa huduma ya uzazi
na mtoto ambayo miundombinu yake kwa sasa ni finyu ikilinganisha na watu mil.
1.5 wanaopata huduma hiyo kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment