Tone

Tone
Home » » MELI FB MATARA ILIYOZAMA ZIWA VICTORIA YAIBULIWA

MELI FB MATARA ILIYOZAMA ZIWA VICTORIA YAIBULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Meli ya FB Matara iliyozama Aprili 17 mwaka huu kwenye Ziwa Victoria imeibuliwa na imehifadhiwa Kisiwa cha Karumo, wilayani Sengerema mkoani hapa.
Meli hiyo mali ya kampuni ya Mkombozi Fishing Marine and Transport ilizama ikiwa na wafanyakazi 10 ambao walinusurika kifo na ilikuwa imebeba tani 280 za sukari yenye thamani ya Sh360 milioni.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Gitano Chacha alisema meli hiyo iliibuliwa baada ya jitihada za wataalamu wa majini kwa kushirikiana na meli nyingine za mizigo.
Chacha alisema meli iliyotumika kuivuta FB Matara ni ya mizigo na ambayo ni abiria maarufu kwa jina la FB Chacha, ikiwa na uwezo wa kubeba tani 400.
“Tumeweza kuibua meli hii baada ya kuzama. Jambo ambalo tunashukuru ni kwamba tumefanikiwa kuitoa na hakuna madhara makubwa yaliyotokea kutokana na ajali hii, licha ya kupoteza sukari iliyokuwamo,” alisema Chacha.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa