Home » » WAPENDEKEZA MFUMO KUPELEKA FEDHA ZA RUZUKU SHULENI UBADILISHWE

WAPENDEKEZA MFUMO KUPELEKA FEDHA ZA RUZUKU SHULENI UBADILISHWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
WADAU wa  elimu wilaya  ya  Ukerewe, Mwanza   wameshauri  mfumo  wa kupeleka fedha  za  ruzuku  shuleni ubadilishwe  ikiwa ni mkakati  wa kudhibiti  matumizi  mabaya  ya fedha hizo.

Wakichangia   taarifa ufuatiliaji wa fedha za  ruzuku shuleni iliyowasilishwa  na shirika  la  Baraka Goodhope Orphans Development [ BAGODE]la  jijini Mwanza  walisema  utaratibu uliopo  unasababisha  urasimu na  hata rushwa.

Mwenyekiti   wa kamati ya  shule  ya  msingi  Kagera  Kasengelema Venance   alisema  kamati  hizo  zinakabiliwa  na changamoto  nyingi  hasa  wakati wa kufuatilia na kupata  fedha  za  ruzuku .

Akifafanua  zaidi  alisema  mbali ya  ufahamu  finyu  juu ya  majukumu  yao pia  alikwenda mbali  zaidi na  kudai kuwa wakati mwingine  wanapewa shinikizo   kupitisha  maripo hewa  kwa manufaa ya  baadhi ya  maofisa  wa elimu ngazi ya  wilaya.

Naye  mchungaji  wa kanisa la  la  TAG   Daniel   Sasita  alisema  ipo haja  ya jamii  kujitizama upya  hasa  juu ya  tatizo sugu  la rushwa  vinginevyo  tutaendelea  kulaumiana  bila  kupata ufumbuzi  wa matatizo  yaliyopo.

Alisema   tatizo  hilo limekita mizizi   kwa kiwango kikubwa  hadi  baadhi ya  watoa huduma hasa  watumishi wa umma wamefikia  hatua  ya kuamiani na  kualalisha rushwa  ya fedha  na hata  ngono kuwa  haki yao. 

Kaimu  afisa  mtendaji  wa  kata ya  Kagera   Joseph  Leo  Mululi  akizungumzia  tatizo  hilo  ametaka   mfumo  uliopo wa  kupeleka fedha  za ruzuku shuleni  ubaliwshwe  ili  kukabili  tatizo hilo la matumizi  hewa ya fedha za  shule.

Alisema  tatizo hilo  mbali ya  kusababisha  maripo  hewa  yanayotokana  na shinikizo  ya baadhi  ya  maafisa  wa idara ya elimu  pia pengine  inaweza  kuwa  sababu kubwa ya  shule kupata  fedha  pungufu.

Awali mwezeshaji  wa  shilika la [ BAGODE ] Hassan  Kilaka  akiwasilisha  taarifa yake  katika  kikao hicho  alisema katika mradi  ufuatiliaji wa matumizi  ya fedha  za ruzuku  shuleni wamebaini  changamoti nyingi ikiwemo  tatizo la kupelekwa fedha  pungufu.

Akifafanua  alisema  tatizo hilo pengine  limekuwa  kikwazo kikubwa  cha  kufikiwa malengo  ya  mpango  wa maendeleo  ya elimu ya msingi  nchini  Mmem   ulianzishwa  zaidi  ya miaka  12 iliyopita.

Mratibu  wa shilika  hilo   Patricia  Kamugisha  alisema lengo la  mradi  huo wa miaka  mitatu  unaotekerezwa  katika  wilaya  tatu  za  Sengerema, Kwimba  na  Ukerewe unalenga  kuinua ufahamu wa jamii  ili iweze kuoji na kusimamia miradi ya maendeleo hasa  fedha  za  ruzuku  zinazopekwa  katika shule za  maeneo yao.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa