Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAUAJI ya vikongwe wilayani Magu, Mwanza yametajwa kuwa chanzo cha
jamii kuishi kwa hofu ya usalama wa maisha yao jambo linalosononesha.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana, aliyasema hayo juzi wakati
wa hafla ya kupokea kituo kipya cha Polisi cha Ngashe-Lugeye,
kilichojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya ANL kwa gharama ya zaidi ya sh
milioni 17 iliyofanyika Lugeye, wilayani hapa.
Alisema mauaji ya vikongwe yanasababishwa na baadhi ya wananchi kuwa
na imani za kishirikina, kwamba baadhi ya vijana wanalipwa fedha kwenda
kufanya mauaji hayo kinyume cha sheria na haki za binadamu.
Chanzo;Tazania Daima
0 comments:
Post a Comment