Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick
Sumaye, amewashauri waliomo kwenye ndoa kuvumiliana katika mambo
mbalimbali ili kuepuka chuki inayoweza kusababisha mauaji.
Sumaye alisema hayo juzi mjini Mwanza wakati wa uzinduzi wa kitabu
‘Furahia Ndoa’ kilichoandikwa na wachungaji Zakayo na Carol Nzogere.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Sumaye alisema kuwepo kwa mifarakano
ndani ya ndoa kunasababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa na ukimwi,
kwa kuwa hutafuta wapenzi nje ya ndoa ama kwa kutimiza haja ya mwili
au kwa kukomoana.
“Familia kuvurugika na watoto kukosa mapenzi ya wazazi huhamia
mitaani, uchumi wa familia kuvurugika na watoto kukosa mahitaji muhimu
ambayo ni elimu, afya na kujifunza tabia mbaya,” alisema Sumaye.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment