Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Walimu (CWT) wilayani Morogoro, kimewataka walimu wote wa
shule za msingi na sekondari wilayani humo kuzisoma mara kwa mara
sheria za utumishi wa umma, kuzielewa na kuzitumia ipasavyo kama ngao
pekee katika wajibu wao kazini na pindi wanapodai haki zao.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu wa chama hicho wilaya, Adam Bayinga,
mjini Mtamba, Tarafa ya Matombo wakati akitambulisha kitengo ‘Ke’
‘Umamawamo’ ndani ya chama hicho na kuhamasisha walimu kujitokeza
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
“Kuna sheria na kanuni zinazoongoza utumishi wa umma, mwalimu ana
mamlaka mbili zinazoweza kumfukuza kazi katika mifumo miwili yaani
kuachishwa kazi na utumishi na bila utumishi…na kuna hatua ambazo
lazima zifuatwe," alisema Bayinga.
Chanzo;tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment