Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka ya jijini Mwanza (Mwauwasa),
inatarajia kutumia euro milioni 104.5, sawa na zaidi ya sh bilioni
238.7 kwa ajili ya kujenga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maji safi
ya kunywa na utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Injinia Anthony Sanga, aliyasema
hayo juzi jijini Mwanza, wakati alipozungumza kwenye uzinduzi wa
maadhimisho ya Wiki ya Maji, yaliyofanyika jijini humo.
Sanga alisema kuwa kati ya fedha hizo, Euro milioni 90 zimetolewa kwa
mkopo na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Uwekezaji ya
Ulaya (EIB), huku Serikali ya Tanzania ikichangia euro milioni 14.5.
Chanzo:Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment