SHIRIKA linalojishughulisha na kutetea haki za wanawake na watoto
jijini Mwanza la TABCO, limeitaka jamii nchini kuwathamini na kuwapa
wanawake haki ya kumiliki mirathi ya wenzi wao.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Shirika hilo la
TABCO, Irene Kyamba, alipozungumza katika semina ya mafunzo ya wajibu wa
kumiliki mirathi wanawake, iliyofanyika ukumbi wa Kisomo jijini hapa.
Alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakinyanyasika na kukosa haki zao
za kumiliki mirathi, pindi mwenzi wake anapofariki dunia, jambo ambalo
halikubaliki.
Irene alisema shirika lake limejiwekea malengo ya kuhakikisha
linaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kuondoa mila potofu
zinazomkandamiza mwanamke kuhusiana na umiliki wa mali zilizoachwa na
mwenzi wake, hivyo ni vema jamii ikabadilika na kumpa haki mwanamke.
“TABCO tumejipanga vizuri kuielimisha jamii iondokane na dhana potofu
na kandamizi kwa mwanamke juu ya umiliki wa mirathi. Tunahitaji kuona
mwanamke anaheshimiwa na kupewa haki stahili ya umiliki wa mirathi.
“Kwa maana hiyo, TABCO hatutarudi nyuma katika juhudi hizi nzuri na
bora kwa ustawi wa jamii na taifa letu. Watoto nao lazima waheshimiwe na
kuthaminiwa,” alisema.
Mwezeshaji wa shirika hilo, Mercy Kaniki, aliisihi jamii kuhakikisha
inamtambua mwanamke kama sehemu muhimu katika nguzo na maendeleo ya
familia
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment