Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imesema
taarifa ya miradi ya maendeleo ya Jiji la Mwanza ni mbaya kuliko za
majiji mengine yote. Hivyo imetoa siku 90 kwa halmashauri hiyo kuandaa
taarifa mpya na sahihi.
Kamati hiyo ipo Mwanza na jana ilikuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji miradi.
Agizo hilo limekuja baada taarifa ya awali
kukataliwa na kamati hiyo iliyokuwa ikifuatilia taarifa ya miradi hiyo
takriban wiki moja iliyopita, bila ya kupata majibu sahihi ya upungufu
kwenye miradi kama ilivyosomwa na Mkurugenzi wake, Halipha Hida.
Akizungumza na watendaji hao, mwenyekiti wa
kamati hiyo, Dk Hamisi Kigwangala alisema wameshindwa kuwawajibisha
watumishi hao ipasavyo, kutokana na kuwa mara ya kwanza kwao kufanya
kazi halmashauri hiyo ambayo haijawahi kufanyiwa ukaguzi tangu kuundwa
kwake.
“Tangu tuanze kufanya kazi kupitia kamati yetu hii
na majiji yote, hatujawahi kuona uandaaji taarifa mbaya kama ya Jiji
la Mwanza,” alisema Dk Kigwangala.
Dk Kigwangala alisema kamati haijapendezwa na
baadhi ya miradi ya ujenzi kituo cha afya ya mama na mtoto, stoo ya dawa
na ofisi ya mganga mkuu inayojengwa.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment