Home » » MSAKO MKALI WA KUSAKA WANAFUNZI WALIOKATISHWA MASOMO KUFANYIKA UKEREWE

MSAKO MKALI WA KUSAKA WANAFUNZI WALIOKATISHWA MASOMO KUFANYIKA UKEREWE

WANAFUNZI   2,990  waliochaguliwa  kujiunga  na elimu wa  sekondari  mwaka huu  katika  wilaya  ya Ukerewe , Mwanza  hadi sasa  awajulikani walipo

Afisa  elimu  wa sekondari wa  wilaya  hiyo  Slivester   Mlimi  ameliambia  baraza la madiwani jana  kuwa  wanafunzi  waliojitokeza na kupokelewa   shuleni  ni  1,775  ambao ni sawa na  asilimia  38 ya  wanafunzi  wote waliochaguliwa kujiunga  na kidato cha kwanza mwaka  huu.

Akielezea ukubwa wa  tatizo hilo  alisema  mbali  asilimia  62 ya wanafunzi waliochaguliwa  kushindwa kujitokeza  pia  wanafunzi  815  waliotakiwa  kuingia  kidato cha tatu  mwaka  huu  hadi  sasa  awajulikani walipo.

Alisema  kati ya  wanafunzi hao  315  hatima yao aijulikani baada ya  matokeo  ya mtiani wa  taifa  wa kuingia  kidato cha tatu  kuzuiliwa  kwa  kushindwa  kulipa  mchango wa  sh.  20,000 kila mmoja, na wengine zaidi  ya 500  hawakufanya  mtiani huo.
Akizungumzia tatizo hilo  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri  ya wilaya  hiyo  Mhamed  Munga   alisema  tayari  ameagiza  wanafunzi  wote  waliochaguliwa  kujinga  kidato cha kwanza   wapokelewe  shuleni  bila  masharti.

Alisema  wakati  wazazi  wanaendelea  kutafuta   ada  na michango mingine  ikiwemo  sare za shule  wanafunzi  hao wanatakiwa  kuwa shule  wakiendelea na masomo  ilimradi  wamepewa  vifaa  vya darasani   kama daftari na kalamu.

Naye  mkuu  wa wilaya  hiyo Mery Tesha    aliyeshutushwa  na suala hilo  ameagiza   hatua  za makusudi  zichukuliwe halaka  ikiwemo  kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba  ili kuhakikisha  wanafunzi wote wanakwenda shule.

Alimtaka  mkurugenzi  awaagize  viongozi  wa ngazi  za  vijiji na kata   wapewe  orodha   ya majina ya wazazi  wanaozuia  na hata kushindwa  kuripa  ada   ya watoto wao   watafutwe  na kufukishwa  mahakani kwa hatua za  kisheria.

Akizungumzia tatizo  hilo lililoelezwa  na baadhi ya madiwani kuwa ni  aibu na fedhea kubwa  mwenyekiti  wa halmashauri  ya wilaya   hiyo  Joseph  Mkundi  amewataka viongozi  na watendaji  katika ngazi zote  kutimiza wajibu  wao.

Alisema  miongoni mwa mambo   waliyokubaliana katika kiako hicho  ni pamoja na  hadi kufikia katikati ya mwezi  huu   viongozi wa ngazi za  vijiji  wawe tayari  wameitisha  vikao pamoja na  mikutano ya  adhala  ikiwa ni  mkakati  wa kukabili  tatizo  hilo.


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa