IDARA ya afya ya halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza imeweka mkakati kabambe wa kuamasishasha na kupata wanachama zaidi ya 10,000 wa mfuko wa afya ya jamii CHF hifikapo Julai mwaka ujao.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ukerewe Dr. Nyanda Kombe amewambia wajumbe wa kikao maalumu cha uzinduzi wa bodi ya afya ya wilaya hiyo kuwa taratibu zilizowekwa zinavuta wananchi wengi kujiunga na mfuko huo.
Alisema tangu julai mwaka jana wanachama wa mfuko huo wameongezeka toka 116 hadi 666 hivyo kukidhi sharti la mfuko huo kupata ruzuku ya fedha toka serikali kuu.
Akifafanua alisema baada fedha ya mfuko huo kuanza kutumika hasa katika ununuzi wa dawa na vifaa tiba tayari wametenga dilisha maalumu la huduma ya dawa kwa wanachama wa mfuko huo.
Alisema utaratibu huo unatolewa katika vituo vyote vya afya vya serikali vya wilaya hiyo unamwezesha mwanacha wa mfuko huo kupata dawa na vifaa tiba bure katika kipindi cha mwaka mzima baada ya kuchangia sh. 10,000.
Akifafanua Dr. Kombe alisema tayari watumishi wote wa idara hiyo wamepewa elimu ya uamasishaji ikiwa ni pamoja na maelekezo ya kutenga dawa za wanachama wa mfuko huo wa CHF ili wanapougua wasikose dawa.
Alisema tayari mikakati hiyo imeonyesha wazi kuvutia wananchi kwa kiwango kikubwa hivyo hadi kufikia Julai mwaka ujao mfuko huo utakuwa tayari na wanachama zaidi ya 10,000 watakao changia zaidi ya sh. Mil. 100.
Mratibu wa mfuko huo Dr. Sadick Mtoigwa alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya kamati za afya katika Zahanati na vituo vya afya kutoa msamaha kwa wachangiaji bila kuzingatia sifa.
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo alisema tangu mfuko huo uanzishwe zaidi ya miaka tisa iliyopita zahanati nane kati 27 zilizopo azijapokea mwanachama hata mmoja wa CHF tatizo ambalo kwa kiwango kikubwa linatokana na usimamizi mbaya wa kamati hizo.
Katika kikao hicho cha uzinduzi wa bodi ya afya pia ulifanyika uchaguzi ambao George Majura alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo huku Revocatus Mtebe akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya hospital ya wilaya hiyo.
Akizindua bodi hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mery Tesha amewataka wajumnbe wa bodi hiyo kutimiza wajibu wao hasa kuamasisha jamii ili ijiunge na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF.
Alisema taratibu zilizopo zinaelekeza iwapo bodi itashindwa kutimiza wajibu wake hivunjwe hivyo ameonya kuwa kama hilo litatokea hatasita kuchukua hatua lengo likiwa kusimamia huduma bora za afya kwa jamii.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment