FAMILA 1,500 katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza zitanufaika na vyandarua vya bure vya kujikinga na ugonjwa wa Malaria vitakavyotolewa na shilika la Lake Victoria Children Centre [ Lvc].
Mwenyekiti wa kamati tendaji wa shilika hilo Alex Magaga amewambia wawakilishi wa shilika hilo ngazi ya kijiji kuwa vyandarua hivyo vyenye thamani ya sh. Mil. 10.8 vitatolewa kwa msaada wa shilika la Kids Aid Tanzania la nchini Ungereza.
Akifafanua alisema shilika lake limepata vyandarua hivyo kupitia mradi wake endelevu wa Heath Action Program [HAP] unaotekelezwa katika vijiji 15 vya wilaya hiyo ukilenga kuongeza elimu ya kinga ya ugonjwa wa Marelia na kupunguza tatizo la utapia mlo.
Akieleza zaidi alisema baada ya mafunzo hayo ya siku moja wawakilishia hao wa LVC katika vijiji hivyo watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa walengwa siku ya kutolewa vyandarua hivyo.
Alisema msaada huo utatolewa kwa familia zenye wanawake wajawaziti na watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwasababu makundi hayo yanahathilika zaidi na ugonjwa wa Malaria.
Mratibu wa LVC Benjamin Mtebe alisema shughuri ya kugawa vyandarua hivyo itaanza kutekelezwa tarehe 24 mwezi hadi Machi 10 hivyo ametaka familia zenye sifa hizo zitambuliwe mapema.
Alisema vyandarua hivyo vitatolewa katika vijiji vya Msozi, Buramba , Nansore, Busiri, Hamkoko na Bukindo vijiji vingine ni Chabilungo, Bwassa, Bukongo, Kakerege, Busunda, Kagera ,Bugorola, Nebuye na kazirankanda.
Mwakilishi wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya hiyo Sophia Simba ameitaka jamii kuachana na imani potofu ikiwa ni mkakati ya kupunguza vifo vya mama na watoto.
Alisema idara yake inakabiliwa na changamoto kubwa katika suala zima la kuamasisha jamii kujikinga na ugonjwa wa Malaria hasa katika matumizi ya vyandarua na unyunyizaji wa dawa majumbani.
Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni baadhi ya watu kutumia vyandarua kukinga bustani na vifaranga vya kuku huku wengine wakipinga nyumba zao kunyunyiza dawa ya ukoko kwa hofu ya kupata ugumba.
Naye mwezeshaji wa mafuzo hayo toka hospital ya wilaya hiyo Vivian Ishengoma amesisitiza matumizi sahii ya vyandarua ili kupunguza mahambukizi ya malaria
Alisema ugonjwa huo ni tatizo kubwa katika wilaya hiyo na kuonya kuwa kama jamii aitaelimishwa vyema vifo vya mama wajawazito na watoto vitaendelea kuongezeka
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment