Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKA la Kimataifa la Help Age Tanzania kwa kushirikiana na Help
Age Germany na Wizara ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Ujerumani (BMZ),
wanatarajia kutumia zaidi ya sh milioni 828.7 kufanikisha mradi wa
kutetea haki za wazee.
Mradi huo umelenga kuinufaisha jamii hiyo ya wazee kutoka wilaya za
Magu na Kwimba mkoani Mwanza na Karagwe na Kyerwa zilizopo mkoani
Kagera kwa vijiji 24, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo.
Hayo yalibainishwa mjini Magu juzi na Meneja wa mradi huo kutoka
Shirika la Help Age International Tanzania, Fravian Bifandimu, wakati wa
uzindizi wa mradi wa haki za wanawake wazee, uliofanyika ofisi za
makao makuu ya shirika la kutetea haki za wazee wilayani Magu, mkoani
Mwanza la Maperece.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment