Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATU
wenye ulemavu jijini Mwanza, wamependekeza katiba mpya ijayo iamuru
rais wa nchi asiteue wabunge watano kutoka kundi hilo maalumu, badala
yake idadi hiyo ipatikane kwa asilimia 30 kati ya wabunge wote.
Mbali na hayo, wamependekeza kuwepo na muundo wa serikali tatu ili
kuipa hadhi na sifa ya kuwa nchi Tanganyika na watu wake, tofauti ilivyo
sasa ambapo imemezwa na Zanzibar.
Mapendekezo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Igombe, Ilemela
Mwanza na watu hao wakati wakichangia hoja kwenye kongamano
lililoandaliwa na Asasi ya Tuamke Disabled Group kwa lengo la kuibua
mambo mapya kwenye katiba mpya.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment