KAMATI ya maendeleo ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza [DCC] imelidhia pendekezo la kuanzinshwa halmashauri ya mji wa Nansio wenye kata 14.
Taarifa ya afisa mipango wa halmashauri ya wilaya hiyo Eliya Kijanga iliyowasilishwa na kulidhiziwa katika kamati ya maendeleo ya wilaya hiyo [DCC] inaonyesha kati ya kata hizo nne ni mpya.
Kata mpya zimetajwa kuwa Bulamba, Malegea, Mgalezi na Muhula huku kata nyingine kumi zikitajwa kuwa ni Bukindo, Namagondo, Kakerege, Nakatunguru, Kagera, Ngoma Nkilinzya, Bukongo, Bukanda na kata ya Nansio iliyopanda adhi na kuwa mamlaka ya mji mdogo tangu mwaka 2004.
Afisa mipango msaidizi , Alex Kabona amekiambia kikao hicho kuwa pendekezo hilo limezingatia vigezo vya kitaalamu ikiwemo idadi ya watu , huduma za kijamii pamoja na vyanzo vya mapato.
Alisema kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 eneo linalopendekezwa kuwa halmashauri ya mji wa Nansio lina wakazi 103,607 hivyo kukithi kigezo cha idadi ya watu.
Alisema kigezo hicho kinataka eneo la halmashauri ya mji liwe na wakazi wasiopungua 30,000 na kuongeza kuwa pia huduma za kijamii kama vituo vya afya , shule za msingi na sekondari , huduma za fedha na mawasiliano vimekidhi vigezo.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa katika eneo la mji huo lenye ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 164,889 pia zipo huduma za mamlaka ya mapato TRA, kituo cha polisi na maduka zaidi ya 50 ya bidhaa mbali mbali.
Katika hatua nyingine kikao hicho pia kimelidhia kata ya Ilangala iliyokuwa na vijiji vinane igawanywe na kupata kata mpya ya Kakukulu wakati huo ikilidhiwa pendekezo la kuanzinshwa vijiji vipya vinne.
Katika pendekezo hilo kata ya Ilangala itabaki na vijiji vya Gallu, Kasenyi, Kamasi na Mulutilima huku kata ya Kakukulu ikiwa na vijiji vya Mibungo, Namakwekwe, Masonga na Kitanga, wakati huo vijiji vipya ni Nampisi, Namakwekwe, Kitanga na Buzegwe.
Mkuu wa wilaya hiyo Mery Tesha alitaka taratibu na kanuni zizingatiwa wakati wa kupitisha mapendekezo hayo ili kuepuka migongano baada ya pendekezo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment