Home » » AZAKI ZATAKA MAJUKUMU YA KAMISHENI WA ARDHI YAREJESHWE NGAZI ZA WILAYA

AZAKI ZATAKA MAJUKUMU YA KAMISHENI WA ARDHI YAREJESHWE NGAZI ZA WILAYA

MTANDAO  wa  asasi za kiraia  katika   wilaya  ya Ukerewe, Mwanza [Ungonet]  wametaka  majukumu ya  kamisheni wa  ardhi  yarejeshwe  ngazi   ya wilaya ili  kupunguza migogoro ya  ardhi.

Pendekezo hilo limetolewa  jana na  wajummbe  wa   mtandao  huo waliokutana  kujadili  tatizo  sugu la  migogoro ya ardhi linaloikabili  wilaya  kwa ufadhili  wa  mtandao wa  kufuatilia sera  wa jijini Mwanza [MPI]

Katika mjadala huo  imeelezwa  kuwa   pengine  suala  la mahamuzi  ya  matumizi ya  ardhi likiamishiwa  ngazi  za wilaya   linaweza kupunguza   migogoro  katika  rasilimali hiyo  muimu  kwa maisha  na maendeleo  ya binadamu.

Mwenyekiti  wa  kijiji cha Kagera  Egisela  Magessa  alisema  utaratibu  uliopo  unaompa mamlaka  kamisheni  wa ardhi  kutoa  ardhi  bila  kuzingatia  matakwa  ya  wananchi   katika eneo  husika   imesababisha  robo  tatu  ya eneo la kijiji hicho  kutolewa  kwa  tasisi  moja  ya  Al-jazira.

Alisema  tatizo hilo nikero kubwa  katika  kijiji hicho  na akaongeza  kuwa  kama  alitapatiwa  ufumbuzi  mapema   hapo baadae  linaweza  kusababisha  vulugu na hata  mauaji  kwa sababu  eneo hilo lilitolewa  bila  kushilikisha  jamii.

Nae  Dimond  Msitta  akiunga mkono  hoja hiyo  alikwenda mbali zaidi  na kutaka utaratibu uliopo unaompa  mamlaka Rais wa  Tanzania  kuwa na  mamlaka ya mwisho katika  ardhi  utazamwe upya.

Akifafanua  alisema  mbali  ya  suala hilo kuwa chanzo cha  migogoro  wa  ardhi  pia  suala  la  kutegemea  mahamzi  ya kamisheni wa  ardhi  aliyeko  Dar-esalamu  kushughurikia  na hata  kugawa  ardhi  ni chanzo kingine cha  tatizo hilo.

Mmoja wa  wawezeshaji , Paul  Benjamin  alisema upanukaji wa makazi , miundombinu , ukame na tishio la jangwa pamoja na  fidia duni pengine  ni sababu  za  kuendelea kushamili  migogoro  ya  ardhi.

Afisa  ardhi  wa halmashauri ya wilaya  hiyo  Elastus  Gwandume  mbali ya kubainisha  sababu kadhaa  ikiwemo upungufu wa wataalamu pia  ametaka  suala la kugawa  ardhi  liangaliwe upya.

Alisema  wakati  inafaamika  wazi  pasipo ardhi  akuna  maendeleo  ya  aina yoyote lakini  gharama za  rasilimali  hiyo ni kubwa na zinaongezeka  kila  kukicha na kusababisha  wananchi wenye kipato  duni   kushindwa kuzimudu.
Akifafanua  Gwandume  ambae sasa ameamishiwa  wilaya ya Rungwe  alikwenda mbali  zaidi  na kutaka   ardhi pia itolewe sawa na huduma nyingine za  kijamii  kama inavyotolewa  huduma za tiba  na  elimu ili kuwawezesha  hata wenye kipado duni kupata  ardhi.

Mwakilishi wa mkuu wa wilaya  hiyo  Casmir Kombo   alisema  tatizo la migogoro ya ardhi ni kubwa  na serikali inaendelea  kulishughulikia na  sasa  inafanya  tathimini  ya ufanisi  wa  mabaraza  ya  ardhi  ya kata na vijiji  na ikithibitika  kuwa   yameshindwa  kutimiza  wajibu wake  yatafutwa.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa