WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, amezitaka
halmashauri nchini kuangalia utaratibu mzuri wa kutenga maeneo ya mifugo
na kuwa wasimamizi ili kuepusha migogoro inayotokea mara kwa mara.
Pia amewataka wafugaji kuwa na sikio sikivu kwa kuwa hakuna aliye
sahihi kati yao na wakulima kutokana na wenzao kuhitaji eneo la kulima
na wao kutaka eneo hilo hilo kwa ufugaji.
Alisema ardhi iliyopo haiongezeki, lakini mahitaji yanaongezeka,
hivyo kuwasihi wafugaji kufuata sheria iliyopo ya ufugaji sambamba na
kuwataka kufuga ng’ombe wa kisasa – mitamba, sambamba na kuwa na
uwekezaji mkubwa unaohitajika.
Dk. Kamani alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye kongamano la
uwekezaji Kanda ya Ziwa alipozungumza na kundi la wafugaji, wavuvi na
sekta zao ambao aliwataka kuwa wabunifu na kuwekeza kisasa, ili kuweza
kupata pato na kujikwamua na umaskini.
Alisema serikali inataka kuhakikisha kuna maeneo ya uwekezaji na
uwezeshaji kufanyika kwa haraka katika maeneo mbalimbali yenye tija
kutokana na kuwa na ng’ombe milioni 22.8, kondoo milioni mbili, kuku
milioni 35 na kwamba idadi ni kubwa ambayo inaweza kuleta tija.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment