SERIKALI
imesema haina mpango wa kutaifisha mali za wawekezaji na kwamba katika
kutekeleza azma ya uwekezaji, haki na mali za pande zote zitalindwa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema hayo wakati akifunga Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa.
Hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
Waziri Mkuu aliwasisitizia wawekezaji kuwa mali zao zitalindwa.
Alitaka
Serikali za mikoa sita ya Kanda ya Ziwa na Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC), kuondoa urasimu usio wa lazima, pale wanapotakiwa kutumiwa katika
kuwawezesha wawekezaji na wananchi kwa ujumla kupata mazingira rafiki
ya uwekezaji.
Waziri
Mkuu aliwahakikishia wawekezaji kuwa serikali itayafanyia kazi maeneo
yote, yaliyoelezwa kama changamoto, ambazo zinakwamisha uwekezaji kwenye
fursa zilizopo, kuanzia zile za sera, kisheria na hata kiutekelezaji.
Akizungumzia
hali ya uchumi, alisema uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa wastani
wa asilimia saba katika kipindi cha hivi karibuni, wakati kilimo kinakua
kwa asilimia nne tu.
Alisema wanahitaji msukumo wa uwekezaji kwenye kilimo ili ukuaji wake ufikie kiwango cha asilimia sita
Chanzo;Habari Leo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment