Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHILIKA la Haki Elimu la
jijini Dar- salamu limeaidi
kuendelea kushilikiana na jamii pamoja na
wadau wengine kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni mkakati
wa kukabili tatizo la kushuka elimu nchini.
Mratibu
wa shilika hilo wilaya ya Ukerewe,
Mwanza Elisante Kitulo alisema hayo jana
wakati anakabidhi vifaa vya kujifunzi vya wanafunzi
wa darasa la hawali katika shule nne
za wilaya hiyo vyenye thamani ya sh. Mil. 1.6.
Katika maelezo
yake amewambia wakazi wa
kijiji cha Mulutanga kuwa mbali
ya shule hizo kupata vifaa hivyo pia shule ya kijiji
hicho imepata motisha ya kujengewa darasa moja
la hawali baada ya kufanya vizuri katika
mtiani wa taifa wa darasa la saba mwaka jana.
Kupitia
mradi huo wa miaka mitano wa
kuimalisha elimu ya hawali unaotekelezwa
katika wilaya 11 nchini pia vimetolewa vitabu
na kuundwa vilabu vya wanafunzi vya
kujisomea hasa masomo ya sayansi na hesabu ikiwa ni mkakati wa
kuvutia wanafunzi kupenda masomo hayo.
Afisa miradi huyo
wa Haki Elimu amesema tayari wajumbe wa kamati za shule
hizo na walimu wa darasa la hawali wamepewa
mafunzo na hivi sasa wanatarajia kutoa
mafunzo kwa walimu wa darasa la hawali
ya kubuni na kutengeneza zana za kujifunzi za wanafunzi
wa hawali.
Akifafanua alisema mradi
huo wa miaka mitano wa kuimalisha elimu ya hawali ulioanzishwa mwaka
2012 unaziusisha shule 88 zikiwemo shule 44
za Sekondari na idadi sawa na hiyo zikiwa shule za msingi katika
wilaya hizo 11.
Mradi huo ulianzishwa
baada ya shilika hilo kufanya utafiti na kubaini idadi ya
wanafunzi wanaitimu elimu ya msingi wakati awajui kusoma na kuandika inazidi kuongezeka
Alisema katika miaka
ya 1980 kuludi nyuma asilimia 90 ya watanzania
waliweza kusoma na kuandika lakini katika miaka ya hivi
karibuni idadi hiyo imeshuka hadi asilimia 40 na kuongeza
kuwa tatizo hilo limeludisha nyuma Tanzania iliyokuwa ikiongoza
kwa nchi za Afrika mashariki na kati kwa idadi kubwa ya
watu wanaweza kusoma na kuandika.
Kufuatia
hali hiyo ameitaka jamii kutambua
na kuwapa msingi mzuri wanafunzi hasa katika elimu
ya hawali ikiwa moja ya mikakati
ya kukabili tatizo hilo.
Wilaya
zinazotekeleza mradi huo zimetajwa kuwa
ni Kilwa, Kilosa, Mvomelo , Mleba, Kigoma, Tabora, Bariadi, Msoma,
Serengeti, Ukerewe pamopja na Arusha mjini
na vijijini.
Ambapo katika wilaya
ya Ukerewe unatekelezwa katika shule za msingi za Nkilizya,
Mulutanga, Nasore na Buzegwe pamoja na shule za sekondari
za Bukongo, Bukindo, Bukanda na Namagondo.
0 comments:
Post a Comment