Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMUIYA ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO),
imeitupia shutuma serikali kwa madai imekuwa ikitengeneza kizazi
chenye elimu dhaifu.
Shutuma hizo zilitolewa jijini Mwanza juzi na Mwenyekiti wa TAHLISO
Taifa, Mussa Mdede, alipozungumzia matokeo ya kidato cha nne.
Mdede alisema kitendo cha serikali kuzalisha wasomi wasiokuwa na
elimu nzuri ni tatizo kubwa kwa taifa, na hali hiyo inaweza kusababisha
wanafunzi kushindwa kufika vyuo vikuu na hata kutofikia kiwango cha
elimu ya kimataifa.
Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Bugando jijini Mwanza, alisema uduni huo wa elimu umekuwa ni mwiba
mkali kwa vijana katika soko la ajira ndani na nje ya nchi, hivyo
lazima serikali ibadili mfumo wake ili iweze kupata wasomi wazuri.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment