Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MASHIRIKA na asasi zisizokuwa za kiserikali kutoka mikoa ya Mwanza
na Geita, wamewaonya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuhakikisha
wanajadili na kupitisha Katiba nzuri inayotakiwa na wananchi ili
kuepusha matatizo yanayoweza kulikumba taifa.
Aidha, imeelezwa Watanzania wengi hawahitaji kurudi kutumia Katiba
iliyopo, badala yake wanataka Katiba mpya inayojali matakwa na masilahi
yao na taifa kwa ujumla.
Onyo hilo lilitolewa jijini Mwanza juzi na washiriki wa warsha ya
jukwaa la Katiba mpya, iliyoandaliwa na Shirika la Kufuatilia Sera
(MPI), la jijini Mwanza na kufanyika ukumbi wa Nyakahoja jijini hapa.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment