Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MASHIRIKA yasiyokuwa ya kiserikali yamelalamikia kitendo cha
serikali kushindwa kusambaza kwa wananchi rasimu ya pili ya Katiba,
jambo ambalo limesababisha Watanzania wengi kushindwa kujua kilichomo.
Wakizungumza jana katika mdahalo wa jukwaa la kujadili mchakato wa
Katiba mpya, ulioandaliwa na Shirika la Kufuatilia Sera (MPI), la
jijini Mwanza, washiriki wa mdahalo huo walisema rasimu ya Katiba ya
Kwanza ilisambazwa na kuifikia jamii kirahisi, tofauti na ilivyokuwa
kwenye rasimu ya pili ya Katiba.
Walieleza hatua hiyo imechangia asilimia kubwa ya wananchi kushindwa
kuelewa maudhui yaliyomo katika rasimu hiyo, hivyo wanaamini hata
wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba hawafahamu maudhui yaliyomo
kwenye rasimu hiyo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment