Misungwi. Kituo cha kuuza mafuta wilayani Misungwi, mkoani
Mwanza, kimefungwa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (Ewura) hadi
kitakapokamilisha ujenzi wa paa.
Kwa mujibu wa barua ya Ewura ya Desemba 13 mwaka
jana iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Miriam Mahanyu inakitaka kituo
hicho kufungwa hadi kikamilishe ujenzi
Mkurugenzi wa kituo hicho, Rashid Nassoro alisema alipokea barua hiyo Januari 24 mwaka huu.
Nassoro aliomba Ewura kumruhusu kuendelea na
huduma, huku akiendelea kukamilisha ujenzi. “Kwa kuwa agizo hili
limekuja tukiwa na akiba ya mafuta ya mwezi mmoja,” alisema.
Baadhi ya wakazi wamelalamikia hatua hiyo, kutokana na kuwa kituo pekee kinachotoa huduma.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment