WATAALAMU kutoka Maabara ya Taifa ya Kudhibiti Ubora wa Mazao ya
Uvuvi, wamesema licha ya kuwa kufanikiwa bado, kuna changamoto
zinazowakabili.
Hayo waliyazungumza jana mbele ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, Dk. Titus Kamani, aliyetembelea maabara hiyo iliyopo mkoani hapa
kujionea hali halisi ya utendaji.
Akielezea changamoto hizo, Ofisa Mfawidhi wa Kitengo cha Kudhibiti
Ubora wa Mazao ya Samaki, Steven Lukanga, alizitaja kuwa ni tatizo la
kukatika kwa umeme mara kwa mara kiasi cha kuwalazimu kutumia jenereta
na ukosefu wa wataalamu wa mitambo ya ukaguzi.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, tangu kuanzisha kwa maabara hiyo mwaka
2003, hawakuwa wanatoza fedha zozote wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi,
lakini kwa sasa wanatoza kiasi cha sh 50,000 kuanzia tani 10.
Mkuu wa Idara ya Kemikali, Longinus Tegulirwa, alisema mitambo
iliyopo katika maabara hiyo ina uwezo mkubwa kwa kupima mazao
mbalimbali licha ya kwamba wateja wa mazao hayo ni wachache.
Kwa upande wake, Dk. Kamani alisema amevutiwa na viwango vya vifaa na
hali ya kuthibitisha ubora, na kwamba ni vema mazao ya samaki wa
Tanzania yawe na ubora wa kutosha ili kuvutia soko la ndani na nje ya
nchi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment